Pata taarifa kuu
UTURUKI-UJERUMANI-USHIRIKIANO

Erdogan aituhumu Ujerumani kuwa na utaratibu wa utawala wa kiimla

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan hatua ya kufuta mikutano ya viongozi wa Uturuki nchini Ujerumani ni utaratibu usitafautiana na ule ulikua ukitumiwa katika zama za utawala wa kiimla.

Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki.
Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Ujerumani walichuku uamuzi wa kufuta mikutano miwili katika miji ya Ujerumani wiki hii, katika sehemu ya kampeni kwa ajili ya kura ya maoni nchini Uturuki Aprili 16, wakati ambapo rasimu ya kumuongezea majukumu Erdogan itawasilishwa.

Ujerumani inawapa hifadhi raia milioni 1.5 wa Uturuki.

"Wajerumani, hamfanyi chochote kuhusu demokrasia na mnapaswa kujua kwamba hatua zenu za sasa hazitofautiane na zile za kipindi utawala wa kiimla," amesema Erdogan katika mkutano wa hadhara mjini Istanbul, nchini Uturuki.

"Hatutaki matendo yao kibaguzi. Tunadhani zama zile zimepitwa na wakati, " Rais Erdogan ameongeza.

Kansela wa Ujerumani bado hajazungumzia rasmi kuhusu kauli hiyo ya Erdogan lakini naibu kiongozi wa chama cha Christian Democratic Union (CDU), cha Angela Merkel, amesema kuwa rais wa Kituruki " amezungumza kama mtoto mkaidi ambaye hakuwezi kupata anachotaka. "

Julia Klockner, ambaye ni naibu kiongozi wa CDU, ameiambia gazeti la Bild: "kulinganisha na utawala wa kiimla inaonyesha hatua mpya za kutovumiliana."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.