Pata taarifa kuu
UFARANSA

Uchaguzi Ufaransa 2017: Fillon afunguliwa mashtaka rasmi, asema hatojiondoa kwenye mbio za urais

Mgombea urais nchini Ufaransa, Francois Fillon, Jumatano ya wiki hii amethibitisha kupewa wito na majaji wa mahakama kuu kuhusiana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, lakini hata hivyo ameapa kuendelea na kampeni.

Mgombea urais nchini Ufaransa, François Fillon, ambaye anakabiliwa na kashfa za ufisadi.
Mgombea urais nchini Ufaransa, François Fillon, ambaye anakabiliwa na kashfa za ufisadi. Christophe ARCHAMBAULT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Fillon mwenye umri wa miaka 62 na aliyewahi kuwa waziri mkuu, alikuwa anapewa nafasi ya kushinda uchaguzi mwanzoni tu mwa mwaka huu baada ya kuomba kupewa nafasi kwenye chama chake cha Republicans mwezi Novemba mwaka jana.

Lakini toka wakati huo amekuwa akikumbwa na kashfa mfululizo kwamba alimlipa mke wake na watoto mshahara kwa kazi ambayo ilikuwa hewa kama wasaidizi wake wakati yuko bungeni.

Fillon amesema kuwa mashtaka dhidi yake yamefunguliwa kwa lengo la kumfanya asitishe nia yake ya kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

"Sitakata tamaa, sitaacha na sitajiondoa," amesema Fillon wakati akizungumza na wanahabari jiji Paris.

Mwendesha mashtaka wa Serikali alianzisha uchunguzi rasmi dhidi yake wiki iliyopita, hali iliyoongeza shinikizo zaidi kwenye kampeni za Fillon, ambaye amekuwa kwenye sintofahamu toka kuibuliwa kwa kashfa hizi.

Hata hivyo Fillon ameendelea kung'ang'ania kuendelea na kampeni zake.

Anavituhumu vyombo vya habari nchini humo kwa kumtoa kafara na kwamba ana amini rais Francois Hollande ameshinikiza uchunguzi dhidi yake ili kumfanya akose sifa za kuwa mgombea.

Tafiti mpya ya hivi karibuni kuhusu kura ya maoni, inaonesha kuwa mgombea mwenye msimamo mkali Marin Le Pen na mgombea mwenye msimamo wa kati Emmanuel Macron ndio wagombea wawili pekee wanaotajwa kuwa huenda wakashinda kwenye uchaguzi wa mwezi April.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.