Pata taarifa kuu
UINGEREZA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Uingereza yakabiliwa na shinikizo la kufuta ziara ya Trump

Zaidi ya watu Milioni moja wametia saini waraka wa kuitaka Uingereza kusitisha ziara ya rais wa Marekani Donald Trump kuja nchini humo.

U.S. President Donald Trump, flanked by Senior Advisor Jared Kushner (standing, L-R), Vice President Mike Pence and Staff Secretary Rob Porter welcomes reporters into the Oval Office for him to sign his first executive orders at the White House in Washingt
U.S. President Donald Trump, flanked by Senior Advisor Jared Kushner (standing, L-R), Vice President Mike Pence and Staff Secretary Rob Porter welcomes reporters into the Oval Office for him to sign his first executive orders at the White House in Washingt Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wamesema kuwa, wamechukua hatua hii baada ya Trump kusitisha raia wanaotoka katika nchi za Kiislamu kuzuru Marekani.

Trump amealikwa Uingereza baadaye mwaka huu, kulihotubia bunge lakini pia kukutana na Malkia Elizabeth wa pili.
Juma lililopita Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alikutana na rais wa Marekani Donald Trump, na walijadiliana kuhusu maswala mbalimbali yanayokumba nchi hizo mbili na dunia.

Kabla ya kukutana na rais Trump, Waziri Mkuu May alisema Uingereza itaendeleza urafiki wake wa karibu na Marekani, lakini alimuonya Trump kuwa karibu sana na Urusi, lakini pia kuendelea kusaidia katika vita dhidi ya ugaidi.

Theresa May ni kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na rais Trump.

Akizungumza mjini Philadelphia, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake nchini MarekaniBi May alisema kwa uhakika nchi yake ambayo ilimaliza uanachama wake kwenye Umoja wa Ulaya, iko tayari kujenga ushirikiano na marafiki zake wa zamani na wapya pia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.