Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAQ-HOLLANDE-UGAIDI

François Hollande: 2017 ni mwaka wa ushindi dhidi ya ugaidi nchini Iraq

Rais wa Ufaransa François Hollande aliwasili mjini Baghdad Jumatatu hii, Januari 2 kwa ziara ya kikazi hasa kwa kuwatembelea wanajeshi wa Ufaransa nchini humo kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugaidi.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande akiongozana na Waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, ahutubia kundi la askari wa Ufaransa waliopo nchini Iraq wakipambana dhidi ya ugaidi.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande akiongozana na Waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, ahutubia kundi la askari wa Ufaransa waliopo nchini Iraq wakipambana dhidi ya ugaidi. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hii, rais Hollande amesisitiza juu ya haja ya kupambana nchini Iraq dhidi ya kundi la Islamic State (IS) kwa "kuzuia vitendo vya kigaidi" nchini Ufaransa.

Rais François Hollande anatarajia kuendelea na majukumu yake mpaka mwisho wa muda wake.
Rais Hollande ambaye ameambatana na waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, wametembelea pia eneo la kaskazini la wakurdi linalojitegemea kiutawala kwenye ziara hii ya siku moja.

"Kuchukua hatua dhidi ya ugaidi hapa Iraq ni sawa na kuzuia matukio mengine ya kigaidi kwenye ardhi yetu," amesema haya wakati akiwa kwenye kambi ya jeshi linalobambana na ugaidi jirani na mji mkuu Baghdad.

Ufaransa ni nchi ya pili kuchangia katika operesheni inayoongozwa na Marekani, ambayo mpaka sasa imetekeleza maelfu ya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za IS kwenye nchi za Syria na Iraq.

Majeshi ya Iraq yalionekana kuelemewa punde tu baada ya wapiganaji wa kijihadi kufanikiwa kuuchukua mji wa Mosul mwezi Juni mwaka 2014.

Rais wa Ufaransa François Hollande amesema muungano wa nchi za Magharibi, kukabiliana na kundi la Islamic State, kutasaidia kuepusha mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa.

Kiongozi huyo wa Ufaransa ametoa kauli hiyo alipowatembelea wanajeshi wa Ufaransa wanaopambana na Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.