Pata taarifa kuu
UFARANSA-URUSI

Ndege za kivita za Urusi zaonekana kwenye anga ya pwani ya Ufaransa

Ndege kuu za kivita za Urusi zimeonekana kwa mara nyingine tena katika anga ya Ulaya. Taarifa hii imetolea na jeshi la Ufaransa. Jumatano jioni, Novemba 16, ndege za kivita aina ya Tupolev 95 zilipita kwenye anga ya kaskazini mwa Ulaya na kisha karibu na pwani ya Ireland na kuingia Ureno, zikipitajuu ya bahari ya Atlantiki kabla ya kugeuza na kurudi nyuma.

Jumatano jioni, 16 Novemba, ndege za Urusi aina ya Tupolev 95 zimeruka kwenye anga ya kaskazini mwa Ulaya (icha ya ndege ya kivita ya Urusi aina ya Tupolev-22M3).
Jumatano jioni, 16 Novemba, ndege za Urusi aina ya Tupolev 95 zimeruka kwenye anga ya kaskazini mwa Ulaya (icha ya ndege ya kivita ya Urusi aina ya Tupolev-22M3). STR / RUSSIAN DEFENCE MINISTRY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Ufaransa ambalo katika miezi ya hivi karibuni lilikuatana mara kadhaa na ndege hizo limetuma ndege ya upelelezi ilikufuatilia ndege hizo za Urusi. Lakini kwa sasa, ndege hizo za Urusi zinaonekana zikiwa mbali kidogo na ardhi ya Ufaransa. Hii ni mara ya tatu tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo jeshi la Ufaransa linakutana na tukio hili.

Februari 17, ndege mbili aina ya Tupolev-160 zilikaribia pwani ya Ufaransa na zilionekana kwenye rada ya ndege za kivita za Ufaransa aina ya Rafale, Septemba 22 ndege hizo zilionekana kwa mara nyingine tena. Jumatano, Novemba 16, ndege tatu aina ya Tupolev 95 na ndege zingine zilionekana juu ya bahari ya Atlantiki. Ndege hizi tatu za zamani za Urusi zina uwezo wa kurusha silaha za nyuklia.

"Tutairusha ndege yetu aina ya Awacs ambayo ina piga kambi magharibi mwa Uingereza ili kuchunguza ndege hizo za Urusi, " amesema jenerali Jean-Christophe Zimmermann, Naibu Mkuu wa shughuli za ulinzi wa jeshi la anga.

Matukio haya yalikuwa yakitokea mara kwa mara wakati wa vita baridi na ndege za Urusi zilionekana kuwa hatari, wamesema marubani wa ndege za kivita za Ufaransa. Kwa sasa, jeshi la anga linafuatilia kwa karibu harakati za Urusi, lakini ndege hizo hazijaingia moja kwa moja katika anga ya Ufaransa. "Hawana nia ya kufanya mashambulizi, "  amesema mmoja wa marubani wa ndege za kivita za Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.