Pata taarifa kuu
UFARANSA

Watu 3 wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kupanga shambulio la kigaidi Ufaransa

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amesema vyombo vya usalama nchini humo vinawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuwa, walikuwa wakipanga njama za kutekeleza shambulio la kigaidi. 

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, ambaye juma hili ametangaza kushikiliwa kwa watu kadhaa kwa tuhuma za ugaidi nchini mwake.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, ambaye juma hili ametangaza kushikiliwa kwa watu kadhaa kwa tuhuma za ugaidi nchini mwake. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa hao wa tatu ni miongoni mwa watu wengine 7 ambao wanashikiliwa kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na mitandao ya kigaidi.

Waziri Cazeneuve amewaambia waandishi wa habari jijini Paris kuwa, Polisi nchini humo imewakamata mamia ya watu kwa tuhuma za ugaidi kuanzia katikati ya mwaka huu na mwaka jana.

Hata hivyo hakuweka wazi taarifa zaidi za watu waliokamatwa hivi karibuni.

Mwezi Agosti mwaka huu, msichana mwenye umri wa miaka 16 alikamatwa kwenye viunga vya jiji la Paris kwenye kitongoji cha Melun ambapo aliwekwa kizuizini kwa tuhuma za kupanga njama za kutekeleza shambulio la kigaidi.

Msichana huyu alikuwa kiongozi wa kundi la kwenye mtandao wa kijamii la Telegram, programu ambayo ilitumiwa na watuhumiwa wawili waliotekeleza shambulio kwenye kanisa moja mjini Normandy mwezi Julai mwaka huu.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazenueve
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazenueve 路透社

Waziri Cazeneuve na mwenzake wa Ujerumani, Thomas de Maiziere, wametoa wito kwa umoja wa Ulaya kutangaza hatua kali dhidi ya watu wanaounda na kutengeneza makundi ya kimtandao ambayo yanatuma meseji za uchochezi kama vile programu ya telegram, iliyotumiwa na msichana aliyekamatwa Ufaransa.

Katika hatua nyingine kijana mwenye umri wa miaka 19 kutoka mji wa Nice, aliyezaliwa kwenye familia ya mashahidi wa Yehova lakini baadae akabadili dini, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kufurahia ugaidi.

Vyombo vya usalama nchini Ufaransa vinapambana na kufanya kila namna kuzuia kutekelezwa kwa shambulio jingine la kigaidi baada ya mashambulizi mawili ya mwezi Julai.

Tarehe 14 Julai, kijana mwenye umri wa miaka 31 mzaliwa wa Tunisia aliendesha gari kwenye mkusanyiko wa watu wakati wa sherehe za Kitaifa za Bastille na kuua watu 68 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 400.

Na tarehe 26 Julai, kijana mwenye umri wa miaka 19 alimkata shingo mchungaji wa kwenye kanisa moja kaskazini mwa mji wa Saint-Etienne-du-Rouvray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.