Pata taarifa kuu
UFARANSA

Moto waua watu 13 kaskazini mwa Ufaransa

Takribani watu kumi na watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya moto kuzuka usiku wa kuamkia jumamosi katika bar moja kaskazini mwa Ufaransa,waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve amethibitisha.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernad Cazeneuve
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernad Cazeneuve BFM : Capture video
Matangazo ya kibiashara

Moto huo ulitokea usiku katika chumba kimoja cha bar wakati sherehe ya siku ya kuzaliwa ikiendelea.

Hata hivyo uchunguzi unafanyika kubaini chanzo cha moto huo.

Afisa mmoja ambaye hakutaja jina lake amebainisha kuwa kuna kila dalili kuwa huenda moja kati ya mishumaa iliyokuwa ikitumika katika sherehe ilisababisha moto huo kushika na kuleta madhara.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amefahamisha kupitia taarifa yake kuwa watu kumi na watatu ndio waliofariki dunia huku wengine sita wakijeruhiwa ambapo mmoja yupo katika hali mahututi.

Afisa mmoja aliyekuwepo eneo la tukio Laurent Labadie alielezea tukio hilo kama ajali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.