Pata taarifa kuu
UTURUKI-EU

Hali ya taharuki katika EU dhidi ya ukandamizaji Uturuki

Mawaziri wa mambo ya Nje wa Ulaya pamoja na John Kerry wamekutana Jumatatu hii Julai 18 katika mkuu wa Ubelgiji, Brussels.

Bango lenye picha ya Rais Tayyip Erdogan wakati wa maandamano ya wafuasi wanaounga mkono Serikal, Ankara, Julai 17, 2016.
Bango lenye picha ya Rais Tayyip Erdogan wakati wa maandamano ya wafuasi wanaounga mkono Serikal, Ankara, Julai 17, 2016. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wameelezea hofu yao juu ya kufunguuliwa upya kwa mjadala kuhusu adhabu ya kifo nchini Uturuki na Rais Recep Tayyip Erdogan pamoja na kukamatwa askari wengi na baadhi ya wafanyakazi katika sekta ya sheria kufuatia jaribio la mapinduzi.

"Leo hii tunasema kwamba utawala wa sheria unapaswa kulindwa kwa manufaa ya Uturuki," amesema Federica Mogherini kwa vyombo vya habari. "Hakuna udhuru kwa Uturuki kuchukua hatua za kuondokana na utawala wa sheria," amesisitiza wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya.

Kamishina wa Ulaya katika masuala ya upanuzi, Johannes Hahn, ambaye anahusika na kuwania kwa Uturuki katika Umoja wa Ulaya, hata hivyo amependekeza kuwa serikali ya Uturuki ilikua iliandaa, kabla hata jaribio hilo la mapinduzi, orodha ya watu watakao wanaotakiwa kukamatwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Didier Reynders, ameonyesha wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa marejesho ya adhabu ya kifo nchini Uturuki, kama alivyozungumza Jumapili mwishoni mwa juma lililopita na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Nchini Uturuki, adhabu ya kifo ilifutwa miaka kumi iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.