Pata taarifa kuu
Ufaransa

Maombolezo ya siku tatu yaanza leo nchini Ufaransa

Ufaransa imeanza kipindi cha maombolezo ya kitaifa leo Jumamosi kwa ajili ya watu 84 ambao waliuawa baada ya gaidi kuendesha lori lake kuelekea kwa umati wa watu mjini Nice wakati wakisherehekea siku ya kitaifa ya mapinduzi.

Baadhi ya waombolezaji mjini Nice
Baadhi ya waombolezaji mjini Nice REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Rais Francois Hollande amesema maombolezo hayo yatadumu kwa siku tatu huku akionya kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka zaidi,wakati huu watu zaidi ya 50 wakiwa katika hali mbaya Kufuatia shambulio hilo Alhamisi usiku.

Dereva wa lori hilo ambaye amesababisha vifo vya watu zaidi ya 80 amebainika kuwa raia wa Tunisia na mhalifu mdogo ambaye baba yake amemwelezea kama mtu asiyependa vurugu ambaye hata hivyo ameathiriwa na msongo wa mawazo huku majirani wakimwelezea kama mtu asiyependa kujichanganya na wengine ambaye hakuonesha dalili za nje za kuwa mfuasi wa Uislam.

Waziri Mkuu Manuel Valls amesema mshambuliaji huyo Mohamed Said Lahouaiej-Bouhlel anawezekana kuwa na ushirikiano na makundi haram ya kiislam, lakini Waziri wa Mambo ya Ndani Bernard Cazeneuve ameonya kuwa ni mapema mno kufanya uhusiano huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.