Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-THERESA MAY

Theresa May achukua hatamu ya uongozi wa nchi

Wajumbe wa chama cha Conservative wanataka kuamini kuwa utulivu umepatikana kwa uteuzi wa Waziri Mkuu mpya anayejulikana kwa jina la Theresa May na kwa sasa kila kitu kitakuwa sawa. Lakini hakuna kilio na uhakika. Katika hali halisi, itakuwa vigumu zaidi.

Theresa May na mumewe Philip May Jumatano Julai 13 watahamia katika makazi ya Waziri Mkuu.
Theresa May na mumewe Philip May Jumatano Julai 13 watahamia katika makazi ya Waziri Mkuu. CHRIS RATCLIFFE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hakika, Theresa May ana matatizo mawili ya uhalali. Kwanza ameingia madarakani kwa mfumo wa ushindani na kuachiana. Hakuchaguliwa, kama ilivyopangwa, na wajumbe wa chama cha Conservative, na jambo jingine hakuchaguliwa na wapiga kura wa Uingereza.

Alikuwa akipinga Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya

Licha ya kupinga Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, sasa inaonekana kwamba Bi May atatekeleza uamuzi wa wananchi wa kujiondoa katika Umoja huo.

Itafahamika kwamba alikua katika kambi iliyokua ikiunga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya kama David Cameron. Theresa May amebainisha kuwa atshikilia wadhifa wake hadi mwaka 2020, tarehe rasmi ya uchaguzi ujao wa bunge. Lakini waangalizi wengi wa kisiasa wanaamini kuwa itakuwa vigumu utofanyika uchaguzi kabla ya tarehe hiyo.

David Cameron, amewaambia Wabunge nchini mwake kuwa, ni lazima nchi yao isalie kuwa karibu na nchi wanachama za Umoja wa Ulaya na jumuiya yenyewe ikiwa wanataka isitetereke baada ya kupiga kura kujitoa kwenye jumuiya hiyo.

Cameron, amesema haya wakati akijibu kwa mara ya mwisho kabisa, maswali ya wabunge, kabla ya kukabidhi ofisi, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Bi. Theresa May, ambaye juma hili alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Conservative.

Wabunge wengi walimpongeza Cameron kwa uongozi wake imara, ambapo kwa sehemu kubwa amefanikiwa kuimarisha uchumi wa taifa hilo katika kipindi cha miaka 6 aliyokaa madarakani.

David Cameron sasa atasafiri kwenda Ikulu ya Buckingham ili kuwasilisha rasmi barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia na kumpendekeza Theresa May kuchukua nafasi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.