Pata taarifa kuu

Slovakia yachukua uwenyekiti wa EU katika hali tatanishi

Baada ya Uholanzi, Slovakia inachukua rasmi Ijumaa hii Julai 1 uwenyekiti wa Umoja wa Ulaya, ambapo ni mwanachama tangu mwaka 2004.

Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker (kushoto), na Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico (kulia) katika mji wa Bratislava tarehe 30 Juni 2016.
Rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker (kushoto), na Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico (kulia) katika mji wa Bratislava tarehe 30 Juni 2016. SAMUEL KUBANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni kwa mara ya kwanza nchi ndogo kama Slovakia kuchukua uwenyekiti wa Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha miezi sita katika hali ya kipekee, wiki moja baada ya kura ya maoni nchini Uingereza.

Changamoto ni kubwa, wakati ambapo Slovakia pia inakabiliwa na kupanda kwa mfumo wa kujitaifisha na kutokua na imani na Ubelgiji.

Brussels haina uhusiano mzuri Slovakia kutokana na ushirikiano wake na vyama vya mrengo wa kulia au upinzani wake mkali kwa kugawana wakimbizi katika kila nchi, kwa sasa ni kwa Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico, ambapo atasimamia moja ya majukumu muhimu.

Miaka kumi na miwili baada ya Slovakia kujiunga na Umoja wa Ulaya pia, mwanachama wa nchi zinazotumia mfumo wa Schengen na sarafu ya euro, inataka kuhakikisha kwamba mustakabali wa Ulaya hauwamuliwi na Berlin au Paris.

"Hata kama umuhimu wa kupokezana uwenyekiti uliyojaa hofu ulipungua kwa kiasi fulani katika miaka ya hivi karibuni, Slovakia ina shinikizo halisi la kuiwakilisha Ulaya ya Kati wakati ambapo inajulikana kama moja ya kundi linalojihusisha na vizuizi ndani ya Umoja wa Ulaya, Martin Michelot, Mkurugenzi wa utafiti kuhusu Ulaya ya Kati katika Taasisi ya EUROPEUM, ametathmini. Na hivyo, katika mwezi Desemba, Slovakia itahakikisha inakuwa maamuzi ya kuweka mbele kama mchango wa kweli wa Ulaya ya Kati kwa muendelezo wa ujenzi wa Ulaya. "

Slovakia kama mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya itajikita na masuala ya kiuchumi, na pia, kwa mujibu wa mpango rasmi, sera ya uhamiaji na hifadhi ya kudumu. Lakini suala la kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya litapewa kipaumble hasa katika mkutano wa kilele wa nchi ishirini na saba, wanacahma wa Umoja wa Ulaya, utakaofanyika katika mji mkuu wa Slovakia katikati ya mwezi wa Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.