Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA

Baraza la Ulaya kukutana baada ya Uingereza kujiondoa katika EU

Baraza la Ulaya linatazamiwa kukutana Jumanne hii, baada ya Uingereza kuamua kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, katika muktadha wa kutafakari jinsi ya kuimarisha uchumi, maendeleo na ushirikiano katika umoja huo.

François Hollande, Angela Merkel na Matteo Renzi wametoa kauli moja Jumatau Juni 27 Berlin, siku nne bada ya Uingereza kujiondoa katika EU.
François Hollande, Angela Merkel na Matteo Renzi wametoa kauli moja Jumatau Juni 27 Berlin, siku nne bada ya Uingereza kujiondoa katika EU. John MACDOUGALL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii Juni 27, Angela Merkel, François Hollande na Matteo Renzi walikutana mjini Berlin kwa maandalizi ya mkutano wa baraza la ulaya ambao unatazamiwa kufanyika Jumanne hii mjini Brussels. Viongozi hao watatu walitoa kauli mmoja ya kupinga mazungumzo na London kabla ya kurasimisha uamuzi wake wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Angela Merkel, François Hollande na Matteo Renzi wameonyesha msimamo pamoja dhidi ya kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Viongozi hao walithibitisha hayo walipokutana JUmatatu hii mjini Berlin. Walisema hakutakuwa na mazungumzo na London kama Uingereza itakua bado haijarasimisha ombi lake la kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kwa Baraza la Ulaya.

Lakini hii haipaswi kuwa kwa sasa. Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alithibitisha Jumatatu hii mbele ya Bunge kwamba hatoiweka matatani Ibara ya 50 ya Mkataba wa Ulaya ambayo imepeleka utaratibu wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya. "Kabla ya kufanya hilo, tunapaswa kuamua ni aina gani ya uhusiano tunataka na Umoja wa Ulaya. Na jambo hilo ni katika majukumu ya Waziri Mkuu anayekuja pamoja na serikali yake kuamua, " David Cameron aliongeza.

François Hollande hataki kupoteza muda

Wakati ambapo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikua akitoa wito tangu ilipopigwa kura ya maoni wa kuwa na "utulivu" na "kujizuia", François Hollande ameomba kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kufanyike kwa haraka. "Wajibu wetu, si kupoteza muda wa kushughulikia suala la kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya" na "kushughulikia suala la mtazamo mpya kwa Umoja wa Ulaya," alisema Rais wa Ufaransa . "Hakuna kitu kibaya zaidi kuliko kutokuwa na uhakika," alisisitiza François Hollande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.