Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA

Wakuu wa EU kujadili mustakabali baada ya Uingereza kujitoa

Waasisi wa umoja wa Ulaya wanataraji kufanya mkutano wa kujadili mustakabali wa kanda hiyo baada ya uamuzi wa Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya na kujiuzulu kwa waziri mkuu David Cameron.

Raisi wa Ufaransa Francois Hollande
Raisi wa Ufaransa Francois Hollande REUTERS/Stephane Mahe
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja na kushuhudia Thamani ya sarafu ya Uingereza, Sterling pound imeshuka kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Baada ya matokeo ya kura ya maoni yaliyoshtusha bara la ulaya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na raisi wa ufaransa Francois Hollande walitoa muongozo wa wito kwa Umoja wa Ulaya kufanya mageuzi ili muungano huo uweze kustahimili baada ya kujiondo akwa Uingereza.

Aidha wakuu wa jumuiya hiyo wameitaka nchi ya Uingereza isichelewe kutoka.
Baadhi ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Ulaya waliotoa maoni yao kuhusu uamuzi uliofanywa na wananchi wa Uingereza, wanataka mchakato wa Uingereza kuondoka ndani ya Jumuiya yao, usichukue muda mrefu kwani kuendelea kuchelewa kutaathiri ukanda wao.

Mkuu wa tume ya umoja wa Ulaya, Jean-Claude Junker, amesema kuwa licha ya hatua ya wananchi wa Uingereza ambao wanapaswa kuheshimiwa kutokana na uamuzi waliouchukua, nchi 27 wanachama zilizosalia zitaendelea kushirikiana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.