Pata taarifa kuu
UGIRIKI-WAKIMBIZI

Zoezi la kuwaondoa wakimbizi katika kambi ya Idomeni kuanza

Zoezi la kuwaondoa wahamiaji na wakimbizi katika kambi ya Idomeni kwenye mpaka wa Ugiriki na Makedonia ambalo limeanza mapema Jumanne hii asubuhi linafanyika "polepole" na "kwa utulivu," Giorgos Kyritsis, msemaji wa Idara ya uratibu wa mgogoro wa uhamiaji , ameliambia shirika la habari la AFP.

Wahamiaji wakipanda basi Machi 23, 2016 Idomeni.
Wahamiaji wakipanda basi Machi 23, 2016 Idomeni. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Operesheni imeanza mapema Jumanne hii asubuhi na linaendelea polepole na kwa utulivu, hakuna ulazimai wa kutumia nguvu," amesema Kyritsis, ambaye alihakikishia Jumatatu wiki hii kwamba zoezi hilo katika kambi hiyo inayowahifadhi watu 8,400 litachukua angalau siku kumi. Waandishi wa habari hawaruhusiwa kuingia katika kambi hiyo Jumanne hii asubuhi, polisi imewazuia kwenye umabli wa kilomita tatu na eneo kunako patikana kambi hiyo, AFP imebainisha.

Kambi ya Idomeni imekua ni eneo muhimu kwa maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanaokwama kufuatia kufungwa kwa kwa barabara zinazoingia katika nchi za Balkan mwanzoni mwa mwezi Machi.

Uamuzi wa kuwaondoa wakimbizi na wahamiaji hao katika kambi hiyo tayari ulisababisha watu 400 kukubali Jumapili kuhamishwa katika kituo cha mapokezi karibu na mji wa Thessaloniki wakati ambapo kundi jingine la watu 400 pia limekua likijandaa Jumatatu usiku kufuatana na kundi hilo la kwanza, kwa mujibu wa polisi wa mji wa Idomeni.

"Tunakaribisha mpango wowote wa serikali ya Ugiriki" wa kuwaondoa wakimbizi na wahamiaji katika kambi ya Idomeni, msemaji wa Tume ya Ulaya, Margaritis Schinas, amesema mjini Brussels Jumatatu hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.