Pata taarifa kuu
UFARANSA-CHIRAC

Laurence Chirac afariki

Binti wa kwanza wa rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac, Laurence Chirac, amefariki kwa ugonjwa wa moyo Alhamisi hii Aprili 14. Alikuwa na umri wa miaka 58.

Laurence Chirac, hapa mwaka 1981 kushoto kwa rais wa zamani Jacques Chirac.
Laurence Chirac, hapa mwaka 1981 kushoto kwa rais wa zamani Jacques Chirac. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na gazetii la Le Point, Laurence Chirac, mwenye umri wa miaka 58, amefariki Alhamisi hii kufuatia mashambulizi ya moyo. Alisafirishwa Jumapili katika hospitali ya mjini Necker baada ya hali yake kuwa mbaya na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Kwa mujibu wa gazeti la Le Point, alifanyiwa matibabu kabla ya kupoteza fahamu na tangu hapo hakuweza kuamka.

Laurence Chirac, alizaliwa Machi 4, 1958, alikuwa ametimiza umri wa miaka 58. Alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya akili tangu alipokua na umri wa miaka 15, na alisadikiwa kufariki mara kadhaa.

Waziri wa zamani Michèle Alliot-Marie, mtu wa karibu wa Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac na mkewe, ameandika ujumbe mfupi kwenye twitter, akitoa rambirambi zake kwa familia ya Chirac.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.