Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UFARANSA-UGAIDI

Mashambulizi: Mohamed Abrini akiri kuwa "mtu mwenye kofia"

Mohamed Abrini, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco, mtuhumiwa mkuu aliekamatwa Ijumaa mjini Brussels, na kufunguliwa mashitaka Jumamosi hii kwa kosa la "mauaji ya kigaidi" ni mtu wa tatu aliekuwepo kwenye uwanja wa ndege wa Brussels, Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imesema.

Viwambo kutoka kamera za ulinzi (CCTV) za uwanja wa ndege wa Brussels, zikionyesha "mtu mwenye kofia," Mohamed Abrini, mtuhumiwa wa tatu wa mashambulizi ya mjini Brussels.
Viwambo kutoka kamera za ulinzi (CCTV) za uwanja wa ndege wa Brussels, zikionyesha "mtu mwenye kofia," Mohamed Abrini, mtuhumiwa wa tatu wa mashambulizi ya mjini Brussels. REUTERS/CCTV/Belgian Federal Police/
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Abrini alikua akiwindwa tangu mashambulizi ya mjini Brussels yaliosababisha vifo vya watu zaidi ya telathini na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.

Mohamed Abrini, alietuhumiwa kuhusika katika mashambulizi ya Novemba 13 katika mji wa Paris na Saint-Denis, amekiri kuwa "mtu mwenye kofia" alienaswa Machi 22 na kamera za ulinzi akiambatana na washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels, Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imetangaza Jumamosi hii.

"Alikubali kuwa alikuwa yeye (...), hakuwa na njia nyingine" baada ya wachunguzi kumuonyesha video, msemaji wa Ofisi ya mashitaka amesema. "Alikabiliwa na matokeo tofauti ya kitaalam na alikiri kuwepo wakati wa mashambulizi hayo. Alieleza kuwa alitupa koti lake kwenye sehemu kunakohifadhiwa takataka na kisha aliuza kofia yake," Ofisi ya mashitaka imesema katika taarifa fupi.

Mohamed Abrini akabiliwa na mashitaka manne

Mahakama ya Ubelgiji imekua ikikamilisha mchakato kamili kwani mashitaka manne yametangazwa mapema Jumamosi hii mchana, ofisi ya RFI mjini Brussels imearifu. Kwanza mashitaka mawili ya "kushiriki katika kundi la kigaidi na mauaji ya kigaidi" dhidi ya Mohammed Abrini na Osama Krayem, mtuhumiwa wa pili alieonekana katika treni za mwendo kasi, na alietambuliwa akiambatana na Khalid el-Bakraoui kabla mtu huyu hajajilipua katika kituo cha treni cha Maelbeek.

Kisha, mashtaka mawili ya "kushiriki katika kundi la kigaidi" na "kushirikiana" kwa mauaji ya kigaidi. Hervé B. M., mwenye asili ya Rwanda, aliekamatwa na Osama Krayem Ijumaa, pia analengwa.

Kwa upande mwingine, mashtaka ya mwisho kuhusu ushirikiano yanamhusu Bilal el-Makhouki ambapo kukamatwa kwake hakujatangazwa. Bilal el-Makhouki alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mwaka jana baada ya kurejea kutoka Syria na ambaye alitoweka mwezi mmoja uliopita, wakati ambapo alikua akifuatilia na bangili ya kielektroniki. Watu hawa wawili waliokamatwa siku ya Ijumaa pamoja na Mohamed Abrini waliachiliwa huru.

Wachunguzi wa polisi ya Ubelgiji wanathibitisha kwamba Osama Krayem ni mtuhumiwa mwingine ambaye alikua akitafutwa. Osama Krayem anatuhumiwa kuwa ndie alinunua mfuko dukani ambao ulitumiwa katika mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.