Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Mahakama ya Ubelgiji yaidhinisha Salah Abdeslam akabidhiwe Ufaransa

media Operesheni ya polisi katika kata ya Molenbeek, Machi 18, 2016, iliyopelekea kukamatwa kwa Salah Abdeslam. REUTERS/Francois Lenoir

Mahakama ya Ubelgiji imechukua uamuzi Alhamisi hii jioni wa kumkabidhi Salah Abdeslam kwa Ufaransa.

Mtuhumiwa muhimu wa mashambulizi ya Novemba 13 katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, alikamatwa katika kata ya Molenbeek Machi 18 baada ya miezi minne akiwa mafichoni na amekua akisema kuwa alitaka "kurudi haraka nchini Ufaransa."

Salah Abdeslam anataka kushirikiana na mamlaka ya Ufaransa, "amejielezea", kwa mujibu wa wanasheria wake. Mtuhumiwa amekubali kujisalimisha kwa Ufaransa.

Mamlaka ya Ubelgiji haikupinga uamuzi huo wa kumkabidhi Salah Abdeslam kwa Ufaransa. Uamuzi wa kitengo cha Mahakama imekua w haraka: baada ya masaa 2 ya kusikilizwa, uamuzi wa mahakama ya Ubelgiji umetolewa. Kikao cha faragha bila kuwepo kwa mhusika mkuu ambaye anazuiliwa katika jela la mji wa Bruges, chini ya ulinzi mkali.

Alhamisi hii asubuhi, mwendesha mashitaka alijielekeza katika jela la mjini Bruges ili kumsikiliza Salah Abdeslam. Itafahamika kwamba Salah Abdeslam, awali alikataa wazo la kutumwa nchini Ufaransa, kabla ya kubadilisha wazo lake baada ya mashambulizi ya mjini Brussels tarehe 22 Machi 2016.

Utaratibu huu wa kibali cha kukamatwa cha Ulaya uko haraka kuliko kutumwa. Salah Abdeslam anaweza kurejeshwa nchini Ufaransa katika siku chache zijazo. Wakati huo atafikishwa mbele ya jaji wa kitengo cha kupambana dhidi ya ugaidi na kufanyiwa uchunguzi. Aliposikilizwa kwa mara ya kwanza nchini Ubelgiji, Salah Abdeslam alikiri kuwa alikua mjini Paris Novemba 13, siku ya mashambulizi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana