Pata taarifa kuu
UHOLANZI-UFARANSA-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Mfaransa anayetuhumiwa kuandaa shambulio akamatwa Uholanzi

Polisi ya Uholanzi imemkamata Jumapili hii mjini Rotterdam (magharibi) raia mmoja wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 32, anaetuhumiwa kuhusika katika maandalizi ya shambulio, Ofisi ya mashitaka imesema, ikibaini kwamba operesheni hiyo imeendeshwa kwa ombi la Ufaransa.

Askari polisi wa Uholanzi wakitoa ulinzi katika kata ya Rotterdam-magharibi, Machi 27, 2016, karibu na mahali ambapo alikamatwa Mfaransa anaetuhumiwa  kuandaa shambulizi pamoja na Reda Kriket.
Askari polisi wa Uholanzi wakitoa ulinzi katika kata ya Rotterdam-magharibi, Machi 27, 2016, karibu na mahali ambapo alikamatwa Mfaransa anaetuhumiwa kuandaa shambulizi pamoja na Reda Kriket. Marten van Dijl / ANP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mfaransa huyo anatuhumiwa kuwa alitumwa na kundi la Islamic State (IS) ili kutekeleza shambulizi nchini Ufaransa pamoja na Reda Kriket, aliekamatwa Alhamisi Machi 24 katika kitongoji cha mji wa Paris, chanzo cha polisi kimesema.

Hati ya kukamtwa ilitolewa na Ufaransa dhidi ya mzaliwa huyo wa jimbo la Paris Desemba 24, 2015 kwa kosa la kushirikiana na wahalifu katika uhusiano na kundi la kigaidi, chanzo hicho kimesema.

"Mamlaka ya Ufaransa, Ijumaa Machi 25, iliomba kukamatwa kwa Mfaransa" ambaye anatuhumiwa "kuandaa shambulizi la kigaidi," Ofisi ya mashitaka ya Uholanzi imebaini mapema katika taarifa yake.

Mtuhumiwa huyo atakabidhiwa kwa Ufaransa "muda mfupi," Ofisi ya mashitaka imeongeza, bila kueleza iwapo mtu huyo alihusika katika mashambulizi yaliyotokea mjini Paris au la.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kata ya Rotterdam Magharibi. Polisi ya Uholanzi pia imewakamata watuhumiwa wengine watatu, ikiwa ni pamoja na watu wawili ambao mmoja ana umri wa miaka 43 na mwengine mwenye umri wa miaka 47, wote kutoka Algeria, kama sehemu ya uchunguzi wa Uholanzi. Hakuna taarifa ambayo imekwisha julikana kuhusu mtu wa tatu aliekamatwa, Ofisi ya mashitaka imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.