Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Ubelgiji yatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 3

media Ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem mjini Brussels, muda mfupi baada ya milipuko, tarehe 22 Machi. REUTERS/Ketevan Kardava/Courtesy of 1tv.ge/Handout via Reuters

Serikali ya Ubelgiji imetangaza Jumanne hii maombolezo ya kitaifa ya siku tatu baada ya mashambulizi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem na katika kituo cha treni za mwendo wa kasi mjini. Mashambulizi ambayo yaliwaua watu 34 kwa ujumla, kulingana na idadi ya muda iliyotolewa muda mfupi uliyopoita.

Maombolezo haya ya kitaifa yatachukua muda hadi Alhamisi jioni, amesema Frédéric Cauderlier, msemaji wa Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel. "Ni maombolezo ya kipekee, bendera zote za kitaifa zitapandishwa nusu mlingoti katika majengo yote ya serikali," ameongeza. Bendera ya taifa kwenye dirisha la afisi ya Waziri Mkuu imepandishwa nusu mlingoti saa saba mchana saa za Ubelgiji (sawa na saa 12:00 saa za kimataifa).

Wakati hayo yakijiri kundi la Islamic State kupitia shirika lake la habari la AMAQ, limekiri kuwa limehusika katika mashambulizi yaliotokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem na katika kituo cha treni za mwendo wa kasi mjini Brussels. Taarifa hii imethibitishwa na tovuti maalum ya Marekaniya SITE.

Mashambulizi hayo yanatokea baada ya siku tatu ya kukamatwa kwa mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris mjini Brussels, Salah Abdeslam. Mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu 130 na wengine wengi kujeruhiwa.

Baada ya mashambulizi hayo katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, nchi kadhaa za Ulaya jirani na Ubelgiji zimeimarisha hatua zao za usalama na udhibiti wa mipaka. Ufaransa, Ujerumani na Uholanzi lakini pia Uingereza zimetangaza masharti mapya mara baada ya mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu 34.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana