Pata taarifa kuu
EU-UGIRIKI-WAKIMBIZI

Wahamiaji waendelea kuingia Ugiriki

Mamia ya wahamiaji wameingia Jumapili katika visiwa vya Ugiriki vya Aegean, siku ya kwanza ya utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Ulaya na Uturuki yanayotakiwa kukomesha mgogoro wa uhamiaji na ambao utekelezaji umeanza vizuri Ugiriki.

Wahamiaji wakiwa nyuma ya mpaka wa nyaya za chuma unaotenganisha Ugiriki na Makedonia, karibu na kijiji cha Idomeni, Machi 2, 2016.
Wahamiaji wakiwa nyuma ya mpaka wa nyaya za chuma unaotenganisha Ugiriki na Makedonia, karibu na kijiji cha Idomeni, Machi 2, 2016. REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili limewaua watu wanne kwa mujibu wa vyanzo vya polisi na mashirika ya kihisani: wasichana wawili wenye umri wa mwaka mmoja na miaka miwili, wamezama baada ya kuanguka kutoka katika meli katika pwani ya kisiwa cha Ro, kusini mwa Aegean, na wakimbizi wawili wa Syria, waliokuwa na maradhi ya presha walipofika katika kisiwa cha Lesbos kaskazini mwa Ugiriki.

Katika janga jingine, wahamiaji tisa kutoka Libya wakielekea Ulaya walikufa maji bada ya kuanguka kutoka katika meli na 600 wengine waliokolewa Jumamosi, aafisa wa Libya wametangaza.

Katika eneo la Lesbos, eneo kuu la kuingia Ulaya kwa maelfu ya wahamiaji wa Syria, Iraq na Afghanistan wanaokimbia vita, polisi imehesabu mchana tu wa Jumapili hii wahamiaji 800 wapya.

Wimbi hili linaweza kuelezwa kwa giza linalotanda bado katika utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Ulaya na Uturuki, amesema mjini Lesbos afisa kutoka Ufaransa wa shirikisho la Ulaya la Mipaka, Frontex.

"Habari hivi karibuni itasambaa kwamba ni vigumu kupita kwa sababu ya makubaliano", ambayo yanaeleza kurudishwa nchini Uturuki wale wote ambao wamewasili nchini Ugiriki Jumapili hii, ikiwa ni pamoja na Wasyria wanaotafuta hifadhi, afisa huyo.

Kwa mujibu wa taasisi ya kuratibu sera ya uhamiaji nchini Ugiriki (Somp), wahamiaji wapyawatawekwa chini ya jinsi makubaliano yanavyoeleza na "hawawezi kuondoka katika visiwa, ambapo watasubiri kuwasili kwa wataalam wa kigeni ambao watazindua taratibu za kurejeshwa kwao. "

Katuka eneo la Lesbos, wamesafurishwa Jumapili mchana katika kituo cha kuorodheshwa cha Moria ambao walikuabado wakisubiri "mwongozo zaidi" juu ya utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Ulaya na Uturuki, kulingana na mkurugenzi wa polisi, Dimitris Amoutzias.

"Wahmiaji wapya wanaorodheshwa kama kawaida. Hatujui bado jinsi mkataba wa kurudisha utakavyotumiwa," Dimitris Amoutzias ameliambia shirika la habar la Ufaransa la AFP.

Msemaji wa Somp Giorgos Kyritsis, alikubali Jumamosi kuwa mipango ya vitendo ilikua bado haijawekwa, wakati ambapo nchi inasusubiri wataalam wa kigeni 2,300 walioahidiwa na kwa washirika wake wa Ulaya kuimarisha zoezi hilo.

Hadi wakati huo, Paris na Berlin wametoa askari 600 na wataalam wa hifadhi, wakati ambapo Rumania imejikubalisa kutuma Jumapili hii wataalam 70.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa hadi tarehe 4 Aprili kuwa zoezi hilo la kwanza liwe limeanza, jambo ambalo Ugiriki haijathibitisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.