Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Mashambulizi ya Paris: Salah Abdeslam akamatwa Brussels

media Operesheni kabambe ya polisi ilianzishwa Ijumaa, Machi 18, 2016 katika wilaya ya Molenbeek, mjini Brussels. REUTERS/Francois Lenoir

Salah Abdeslam, mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris, amekamatwa Ijumaa hii Machi 18 katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, vyanzo vya polisi vikinukuliwa na shirika la habari la Ufaransa la AFP, vimesema.

Alama za vidole vyake zimepatikana katika ghorofa iliofanyia msako na vikosi vya polisi vya Ubelgiji na Ufaransa Jumanne Machi 15.

Salah Abdeslam anakamatwa baada ya kusakwa kwa kipindi cha miezi minne. mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Novemba 13 katika mji wa Paris amekamatwa jumaa hii Machi 18 katika wilaya ya Molenbeek mjini Brussels wakati wa operesheni kababme ya polisi. Kwa mujibu wa vyanzo vya polisi vikinukuliwa na shirika la habari la la Ufaransa la AFP, mtu mmoja amjeruhiwa.

Operesheni ya kumkamata Abdeslam Salah imeanzishwa baada ya msako wa Machi 15 katika eneo la Forest, kitongoji cha Brussels, ulioendeshwa na vikosi vya polisi vya Ubelgiji na Ufaransa. Wakati wa operesheni hii, maafisa wa polisi wanne wamejeruhiwa, wakati ambapo mtu mmoja ameuawa na vikosi vya usalama. Inasadikiwa kuwa ni mmoja wa watuhumiwa waliohifadhi vifaa vya mashambulizi. "Mohamed Belkaïd alieuawa katika eneo la Forest Jumanne wiki hiini ni mmoja wa washirika wa Salah Abdeslam. Alitumia jina la uongo la Samir Bouzid. Huu ni mmoja watuhumiwa waliohifadhi vifaa vilivyotumiwa katika mashambulizi ya Paris, " shirika la utangazaji la RTBF limeangika katika tovuti yake.

Vinasaba vya damu vya Abdeslam vilipatikana katika mabaki

Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imethibitisha Ijumaa hii mchana kwamba alama mbili za Salah Abdeslam ziligunduliwa katika nyumba moja. Kuna kwanza vinasaba vya damu lakini pia alama ya vidole. alama ya vidole imepatikana kwenye kioo kichafu kilichotokana na risasi au urushianaji risasi mara tatu uliotokea kati ya kuwasili kwa wachunguzi kwa ajili ya msako walidhani kuendesha kila mara na wakati ambapo mtu anayeshukiwa kuwa mwanajihadi wa mwisho alipigwa risasi na askari polisi mzoefu.

Salah Abdeslam anaweza kuwa mmoja wa watu wawili ambao walikimbia wakipitia kwenye paa wakati wa mchana kabla ya kutoweka, na tangu wakati huo walianza kusakwa na polisi nzima ya Ubelgiji na Ufaransa. Itafahamika kwamba Ofisi ya mashtaka imekataa kutoa maelezo yoyote yanayohusiana na taarifa hii.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana