Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

EU yakubaliana juu ya msimamo wa pamoja dhidi ya wahamiaji

media Viongozi wa Ufaransa Hollande, Ugiriki Alexis Tsipras na Ujerumani Angela Merkel wamejaribu kuendeleza mkataba kwa kutafutia suluhu mgogoro wa wahamiaji katika bara la Ulaya, pamoja na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya. REUTERS/Stephane de Sakutin/Poo

Viongozi wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya wamekamilisha "msimamo wa pamoja" Alhamisi hii, Machi 17 kwa ajili ya makubaliano na Uturuki yenye lengo la kukabiliana na kumiminika kwa wahamiaji barani Ulaya, Waziri Mkuu wa Luxembourg Xavier Bettel amesema.

Lengo ni kukamilisha maelezo ya mkataba wenye lengo la kuzuia kumiminika kwa wahamiaji barani Ulaya. Makubaliano ambaye maudhui yake yalielezwa wiki mbili zilizopita.

Kuna "makubaliano juu yamsimamo wa Umoja wa Ulaya", na Rais wa Baraza la Ulaya DonaldTrump "atayawasilisha kwa Waziri Mkuu wa Uturuki kabla ya kikao chetu cha Baraza la Ulaya" ambacho kinaendelea Ijumaa hii, Xavier Bettel amebaini kwenye akaunti yake Twitter.

Katika mapendekezo ya mpango uliowekwa, wahamiaji wanaoingia Ugiriki kutoka Uturuki watarudishwa huku Uturuki ikipewa msaada wa kifedha na wakati huo huo raia wake kuweza kuingia barani ulaya bila visa.

Rais wa Ufaransa François Hollande amesema, kwa upande wake, usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa mjini Brussels kwamba hawezi "kuhakikisha matokeo ya mafanikio" ya majadiliano kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki juu ya udhibiti wa wahamiaji "siwezi kuwahakikishia kwamba kutakuwa na hitimisho lenye mafanikio (katika majadiliano) ambayo yatahitajika kwa wakimbizi, Ulaya na Uturuki. "

Rais wa Ufaransa, François Hollande, amesema kunahitajika makubaliano ambayo yataisaidia Ugiriki pamoja na Uturuki.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alilizungumzia baada ya mkutano huo wa umoja wa ulaya na Uturuki uliofanyika nchini Brussels.

Amesema Uturuki imekubali kukabiliana na wimbi la wahamiaji kwa kupokea wakimbizi ambao wanarudishwa kutoka Ugirikri, fursa ambayo ni nzuri ili kwa kuwa inawaweka pembeni wafanya biashara haramu wa binadamu.

Hata hivyo suala hili linapaswa kuwa wazi kisheria, suala ambalo lilipewa mkazo zaidi katika mkutano huo.

Itakumbuka kwamba, rasimu ya makubaliano na Uturuki ilikua inatoa mambo kadhaa:

► kuongeza mara dufu kiasi cha Dola bilioni 3 (ambazo tayari zimetengwa kwaz ajili ya wahamiaji nchini Uturuki)

► Kufuta, kuanzia majira haya, mahitaji ya visa ya muda mfupi kwa raia wa Uturuki wanaoelekea Ulaya

► kubadilishana kati ya mhamiaji na mkimbizi, ikimaanisha mhamiaji alieingia kinyume cha sheria nchini Ugiriki 9 kumrejesha Uturuki) dhidi ya mkimbizi anaeishi nchini Uturuki( kwa kwenda Ulaya)

► kuongeza kasi ya mazungumzo kwa ajili ya kuingizwa kikamilifu kwa Uturuki katika Umoja wa Ulaya.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana