Pata taarifa kuu
UTURUKI-PKK-SHAMBULIO

Uturuki: watu kadhaa wakamatwa baada ya shambulio Ankara

Polisi ya Uturuki Jumatatu hii, imewakamata watuhumiwa kadhaa siku moja baada ya shambulio la kujitoa mhanaga la bomu lililotegwa ndani ya gari, ambalo liliwaua watu wasiopungua 36 katikati mwa mji wa Ankara, kwa mujibu wa serikali.

Mmoja wa waathirika wa shambulio la kujitoa mhanga la bomu lililotegwa ndani ya  gari, Machi 13, 2016 Ankara, akisafirishwa kwenda hospitali katika mji mkuu wa Uturuki.
Mmoja wa waathirika wa shambulio la kujitoa mhanga la bomu lililotegwa ndani ya gari, Machi 13, 2016 Ankara, akisafirishwa kwenda hospitali katika mji mkuu wa Uturuki. OZAN KOSE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa chama cha PKK wananyooshewa kidole kuhusika na shambulio hilo.

Masaa kdhaa baada yashambulio hilo, ndege ya jeshi la Uturuki iliendesha mashambulizi ya kulipiza kisasi katika ngome kadhaa za waasi wa PKK katika milima ya kaskazini mwa Iraq, hasa karibu na maeneo ya Kandil na Gara, uongozi wa jeshi la Uturuki umetangaza.

Watu wanne hadi watano wamekamatwa pia katika mji wa Sanliurfa, Kusini-Mashariki, mji wenye wakazi wengi kutoka jamii ya Wakurdi ambapo kulinunuliwa gari iliyotegwa bomu, ambayo ililipuka Jumapili usiku dhidi ya basi ndogo katika eneo linalotembelewa na watu wengi la Kizilay.

Pigo hili mpya lililotokea katikati mwa mji wa Ankara,shambulio la pili ndani ya kipindi kisizidi mwezi moja, linamuweka hatarini Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye chama chake kilishinda uchaguzi wa wabunge Novemba 1, huku akiahidi "kutokomeza" kundi la waasi wa Kikurdi na kukabiliana dhidi ya "machafuko".

Hakuna kundi hata moja lililodai kuendesha mashambulizi ya Jumapili usiku, lakini serikali ya Uturuki iliharakia kuwanyooshoea kidole "magaidi" wa Kikurdi.

"Tunaamini kwamba mmoja wa washambuliaji ni mwanamke mwenye uhusiano na kundi la PKK," amesema kwa masharti ya kutotajwa jina afisa wa Uturuki, akiliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, Seher Cagla Demir, mwenye umri wa miaka 24, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Balikesir (kaskazini magharibi), ametambuliwa kutokana na alama za vidole vyake.

Februari 17, shambulio la kujitoa mhanga la bomu lililotegwa ndani ya gari, ambalo lilidaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji la PKK, lililolenga magari yaliokua yakiwasafirisha wanajeshi liliwaua watu 29.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.