Pata taarifa kuu
EU-UTURUKI-WAHAMIAJI

Uhamiaji: Uturuki yaomba EU Euro bilioni tatu za ziada

Uturuki imeomba Umoja wa Ulaya Euro bilioni tatu za msaada wa ziada "ifikapo mwaka 2018", sawa na bilioni sita kwa jumla.

Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk na Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz, Brussels, Machi 7, 2016.
Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk na Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz, Brussels, Machi 7, 2016. THIERRY CHARLIER/POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Pia Uturuki imeahidi kwa kiasi kikubwa kuongeza ushirikiano wake katika mgogoro wa wahamiaji ili kukabiliana na ongezeko la wahamiaji, Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz amesema Jumatatu hii.

"Fedha hizi za ziada zitahitaji taratibu za bajeti za ziada. Bunge la Ulaya likotayari kuharakisha taratibu," Schulz amesemakatika mkutano wa kilele wa EU-Uturuki mjini Brussels, ambapo Ankara imeonekana tayari kukubali kurudi kwa wahamiaji wengi, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Syria.

Umoja wa Ulaya tayari umekubali kuisaidia Uturuki hadi kitita cha Euro bilioni tatu kwa ajili ya miradi ya kukuza ushirikiano wa wakimbizi milioni 2.7 wa Syria katika ardhi ya Uturuki, kwa elimu ya watoto katika lugha ya Kiarabu au kuwapatishia ajira kwa mfano, kama sehemu ya mpango wa utekelezaji wa pamoja uliosainiwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2015.

Lakini mpango ni mgumo kueleza iwapo utapelekea kushuka kwa kiasi kikubwa kwa kuwasili kwa wakimbizi kwenye pwani za Ugiriki wakitokea Uturuki. Jumapili hii jioni, Ankara imetoa mfululizo wa mapendekezo, ikiahidi kuwachukua, kuanzia tarehe 1 Juni, wahamiaji wa kiuchumi ambao iliwaacha waingiye Ulaya, ili iweze kuwarejesha katika nchi zao, lakini pia wakimbizi wa Syria.

Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya imejikubalisha kuwezesha mifumo ya kisheria ya wakimbizi wa Syria katika umoja huo, moja kwa moja kutoka Uturuki, kwa idadi kubwa.

Uturuki inahitaji mambo mengine muhimu: pia inataka viza ya bure kwa raia wa Uturuki ianze kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni na inataka mazungumzo ya kujiunga na umoja wa Ulaya, yaliosimama kwa zaidi ya muongo mmoja, yaanzishwe upya haraka iwezekanavyo kutokana na ufunguzi wa sura mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.