Pata taarifa kuu
EU-UGIRIKI-WAKIMBIZI

EU yatenga Euro milioni 700 kwa nchi zinazokabiliwa na wimbi la wahamiaji

Huu ni mradi wa kipekee uliozinduliwa na Tume ya Ulaya wa kutenga kitita cha Euro milioni 700 kwa lengo la kukabiliana na mgogoro wa wahamiaji.

Mkimbizi huyu akimesimama mbele ya uzio wa nyaya za chuma unaoashiria mpaka kati ya ugiriki na Makedonia katika eneo la Idomeni, Machi 2, 2016.
Mkimbizi huyu akimesimama mbele ya uzio wa nyaya za chuma unaoashiria mpaka kati ya ugiriki na Makedonia katika eneo la Idomeni, Machi 2, 2016. REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Kitita hiki kitapewa Jumla ya nchi wanachamazinazokabiliana kwa mstari wa mbele na wimbi la wahamiaji, kama vile Ugiriki, nchi ambayo watu 10,000 bado wanazuiliwa katika mpaka wa Makedonia, na wanakabiliwa na hali ngumu mno. Hii ni ishara ya kipekee, lakini inaibua maswali mengi.

Tume ya Ulaya itatoa milioni 700 hadi mwisho wa kipindi cha bajeti cha miaka saba, ni kusema kwamba, kwa mwaka huu, na miaka miwili inayofuata.

Karibu nusu ya fedha hii itakuwa kupatikana mara moja. Uamuzi huu sambamba takribani kwa wote uharaka na hamu ya upande Kigiriki.

EU yaikumbuka Ugiriki

Hakika, Ugiriki inaonekanakuwa haina uwezo wa kukabiliana na wingi wa wakimbizi waliowasili kwenye ardhi yake. Kambi ya Idomeni, katika mpaka na Makedonia, unaeleza wazi mahitaji ya nchi hii. Kambi hii ina uwezo wa kupokea wakimbizi 1,600, lakini kwa sasa ina wakimbizi 10 000. Matatizo yameendelea kuongezeka licha ya kuingilia kati kwa mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali na na yale ya kujitolea, hali imerudi kuwa mbaya zaidi.

Kuna haja ya kuanzisha miundombinu na wafanyakazi kwa kuwapatishia hifadhi na kuwahudumia chakula wahamiaji. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wakimbizi 24 000 wamepewa hifadhi nchini Ugiriki na nchi ni inajiandaa kuwapokea wakimbizi wengine 100 000. Ugiriki iliwasilisha hivi karibuni mpango wa dharura kwa Tume ya Ulaya ikikadiria mahitaji yake ya kifedha kwa Euro milioni 480. Tume, kwa kuepuka mgogoro wa kibinadamu baada ya kufungwa kwa mpaka wa Makedonia, imependekeza kutenga sehemu ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Ulaya, ambayo mpaka sasa imekua imehifadhiwa kwa ajili ya nchi za ulimwengu wa tatu. Misaada ambayo ilifikia kwenye kiwango cha zaidi ya Euro bilioni moja kwa nchi za Ulaya zinazozidiwa na wingi wa wahamiaji ikiwa ni pamoja na Ugiriki.

Lakini hata hivyo jambo hili liinaibua maswali mengi na utata. Kwanza, mpaka sasa fedha hizi zilikua zimehifadhiwa kwa ajili ya oparesheni za kibinadamu katika nchi ambazo si wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kamishna wa misaada ya kibinadamu, Chypriote Christos Stylianides, amebaini kwamba fedha hizi hazikutengwa kwa miradi iliyopo, ukweli ni kwamba fedha hizi zitasaidia Ugiriki na nchi nyingine zinazokabiliwa kwa mstari wa mbele na wimbi la wahamiaji ili ziweze kujidhatiti vilivyo na hali hii.

Kwa upande mwingine, kuna suala la matumizi ya fedha hizi. Kawaida, Umoja wa Ulaya unashugulikia katika nyanja ya kibinadamu kupitia mashirika yasio ya kiserikali. Lakini hapa, Athens inaonekana kutaka kuchukua moja kwa moja usimamizi wa ujenzi wa nyumba au kambi zitakowahifadhi wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.