Pata taarifa kuu
UGIRIKI-BULGARIA-MAANDAMANO-KILIMO

Mpaka kati ya Ugiriki na Bulgaria wafungwa

Mpaka kati ya Bulgaria na Ugiriki umefungwa pande zote mbili. Madereva wa malori wameghadhabishwa dhidi ya vizuizi vya barabarani vya wakulima wa Ugiriki ambao wamezuia maeneo ya mipaka wakipinga dhidi ya mageuzi ya mfumo wa pensheni katika nchi yao.

Foleni kubwa ya malori karibu na mpaka kati ya Bulgaria na Ugiriki.
Foleni kubwa ya malori karibu na mpaka kati ya Bulgaria na Ugiriki. REUTERS/Stoyan Nenov
Matangazo ya kibiashara

Ghafla, wamezingira maeneo sita ya mipaka kati ya nchi hizo mbili. Hali ya taharuki imetanda na, kwa sasa, hakuna ufumbuzi unaonekana kupatikana.

Njia zote zinazoingia na kutoka kati ya Bulgaria na Ugiriki zimefungwa tangu Ijumaa hii asubuhi. Maeneo madogo ya mipakani, ambapo ni vigumu kwa malori kupita, yameendelea kufungwa. Kufungwa kwa maeneo hayo kumesababishwa na kushindwa kwa mazungumzo kati ya Wabulgaria na Wagiriki katika ngazi zote.

Kwenye eneo kuu la mpaka wa Kulata-Promachonas, uliyoko kilomita 200 kusini mwa mji wa Sofia, foleni ya malori imefikia kwenye kilomita thelathini. Mapungufu katika makampuni ya usafiri yamefikia milioni 10.

Masoko ya Bulgaria pia yanakabiliwa na mgogoro: ukosefu wa matunda na mboga kutoka Ugiriki umesababisha kupanda kwa bei kutoka 30 hadi 40%.

Hali ya taharuki pia imepanda kwa sababu ya hali ya maisha mpakani. Watumiaji wa barabara zilizofungwa wanapaswa kutembea kilomita kadhaa ili kupata maji na chakula.

Kwa upande wake, serikali ya Bulgaria inaunga mkono harakati za watumiaji wa barabara. Waziri wa Uchukuzi Ivaylo Moskovski amesema kuwa serikali ya Ugiriki na wakulima hawakuheshimu ahadi yao ya kutoa haki ya dharura ya kutumia baadhi ya barabara kwa malori ya Bulgaria. Pia ametangaza "kutojadili na wakulima wawanyonge, wakati ambapo serikali ya Ugiriki ilijiuzulu."

Mji wa Sofia unatarajia kuomba fidia kwenye Umoja wa Ulaya, wakati ambapo Bunge la Bulgaria likitoa wito kwa serikali ya Ugiriki kuingilia kati masuala ya wakulima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.