Pata taarifa kuu
Ufaransa-UTEUZI-SIASA

Ufaransa: Jean-Jacques Urvoas Waziri mpya wa Sheria

Waziri wa Sheria nchini Ufaransa Christiane Taubira amejiuzulu kwenye wadhifa huo, baada ya kupinga marekebisho ya Ibara ya Katiba kuhusu kunyan'ganywa uraia wa Ufaransa kwa raia waliozaliwa nchini humo ambao wazazi wao ni kutoka mataifa ya kigeni iwapo watakutikana na hatia ya makosa yanayohusiana na ugaidi.

Waziri mpya wa Sheria wa Ufaransa, Jean-Jacques Urvoas, hapa ni Februari 18, 2015.
Waziri mpya wa Sheria wa Ufaransa, Jean-Jacques Urvoas, hapa ni Februari 18, 2015. AFP PHOTO/ PATRICK KOVARIK
Matangazo ya kibiashara

Kwenye wadhifa huo ameteuliwa Jean-Jacques Urvoas, ambaye ni Mwanasheria na Mtaalamu wa maswala ya polisi na Ujasusi. Waziri mpya wa Sheria ni mshirika wa karibu wa Waziri Mkuu Manuel Valls.

Kipaumbele chake kitakuwa kusaidia Waziri mkuu kupitisha mageuzi ya Katiba, kuhusu kunyimwa kunyan'ganywa uraia wa Ufaransa kwa raia waliozaliwa nchini humo ambao wana uraia wa kigeni, watakao kupatikana na hatia ya makosa yanayohusiana na ugaidi.

Muda mrefu Jean-Jacques Urvoas alifikiriwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, lakini ameteuliwa Jumatano hii Januari 27 na Rais Hollande kumrejelea Christiane Taubira, ambaye amejiuzulu kwenye wadhifa wa Waziri wa Sheria.

Jean-Jacques Urvoas, mwenye umri wa miaka 56, ni baba wa watoto wawili, Mwanasheria na Mtaalamu wa maswala ya Polisi na Upelelezi - kama Manuel Valls - pia aliwahi kuwa Katibu wa kitaifa kwenye wizara ya Usalama mwaka 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.