Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI

Mwanafunzi mwenye asili ya Uturuki amshambulia mwalimu wa Kiyahudi

Mwanafunzi wa shule ya sekondari mwenye asili ya Uturuki, ambaye hajulikani na Idara ya Ujasusi ya Ufaransa, Jumatatu hii, amemshambulia na kumjeruhi mwalimu wa Kiyahudi, akisema wakati alipokua akihojiwa na polisi kuwa amefanya hivyo kwa "jina la Mwenyezi Mungu" na kwa niaba ya kundi la IS.

Maafisa wa polisi wakitoa ulinzi mbele ya shule la Kiyahudi "La CSource" baada ya shambulio la mwalimu, Januari 11, 2016, Marseille.
Maafisa wa polisi wakitoa ulinzi mbele ya shule la Kiyahudi "La CSource" baada ya shambulio la mwalimu, Januari 11, 2016, Marseille. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kijana, ambaye atatimiza miaka 16 katika siku zijazo, amemjeruhi kwa panga mwalimu wa Kiyahudi, mwenye umri wa miaka 35, ambaye alikuwa njiani akielekea kazini mapema Jumatatu hii asubuhi.

Muathirika ameshambuliwa kwa mara ya kwanza mgongoni, kisha akaanguka. Kijana huyo aliendelea kumshambulia mwalimu ambaye amekua akijihami kwa miguu yake, mwendesha mashitaka wa Marseille, Brice Robin, amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Kijana alikuwa na sura ya "kutisha" na nia yake ilikuwa "kuua", kulingana na kauli ya muaathirika, lakini hakuweza kuzungumzia, Robin ameongeza. Panga lililotumiwa kwa kumjeruhi mwalimu huyo wa Kiyahudi halikua na ukali, na hivyo kupunguza kiwango cha majeraha. Mwalimu huyo amepata majeraha madogo mgongoni na mkononi.

Mshambuliaji amekamatwa dakika chache baadaye. Mbele ya polisi, "alidai kuwa alifanya hivyo kwa jina la Allah na kwa niaba ya kundi la Islamic State", mwendesha mashitaka amesema. nchini Iraq na Syria, Wakurdi wako miongoni mwa vikosi ambavyo vinapambana dhidi ya kundi la IS.

Rais François Hollande amelaani vikali kitendo hicho, ambacho hakina "tafsiri yoyote". Hollande amesema kuwa anaungana na "muathirika pamoja na ndugu zake". Amesisitiza kwamba "uhamasishaji wa mamlaka ya umma kwa kuchukua hatua na zinazohitajika dhidi ya kupambana na Uyahudi na ubaguzi wa rangi".

Uchunguzi umeanzishwa katika mji wa Marseille kuhusu "jaribio la mauaji mabaya zaidi kwa sababu ya mtu kuwa na dini yake" na "kutetea ugaidi". Ofisi ya mashitaka dhidi ya ugaidi ya mji wa Paris, Jumatatu hii jioni, imekubali kuendesha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.