Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Ufaransa: heshima ya Jamhuri kwa wahanga wa mashambulizi ya 2015

media Rais Hollande, Waziri Mkuu Manuel Valls na Meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo, Jumapili hii, Januari 10, 2015 mbele ya mnara wa kumbukumbu wa eneo la Jamhuri, Paris. REUTERS/Philippe Wojazer

Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwanamuziki mashuhuri Johnny Hallyday wametoa heshima zao za mwisho kwa wahanga wa mashambulizi ya mwaka 2015 yaliyoendeshwa na kundi la magaidi katika mji wa Paris na maeneo mengine nchini Ufaransa.

Mamia ya maelfu ya raia wamekusanyika Jumapili hii Januari 10 katika eneo la Jamhuri ili kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya mwaka 2015.

Sherehe hiyo imefanyika chini ya ulinzi mkali. Maelfu ya watu wamehudhuria sherehe hiyo katika eneo la Jamhuri, ambapo imekuwa, katika muda wa mwaka mmoja, ishara kwa taifa nzima la Ufaransa. Eneo hili la katikati ya mji mkuu wa Ufaransa hatimaye ni eneo la kumbukumbu. Watu wamemiminika kwa wingi Jumapili hii, tofauti na maandamano ya raia mwaka mmoja uliopita, Januari 11, 2015. mwanamke mmoja aliyekuwa eneo hilo amesema: "Baada ya mashambulizi, tulikuwa katika masikitio na machonji. Leo, Sherehe imekuwa rasmi, na mengi tumeyasahau yaliotokea mwaka 2015, licha ya kuwa tutaendelea kuwakumbuka ndugu zetu walioangamia katika mashambulizi ya magaidi. "

Rais wa Jamhuri na Meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo wamezindua sherehe hiyo kwa heshima ya "watu wa Ufaransa" katika eneo la Jamhuri, ambalo baada ya mwaka mmoja limekua eneo la kumbukumbu.

Mbali na rais wa Ufaransa na Bi Hidalgo, Manuel Valls, mawaziri kadhaa ikiwa ni pamoja na Bernard Cazeneuve (wa Mambo ya Ndani), Christiane Taubira (wa Sheria) na Fleur Pellerin (wa Utamaduni), walikuwepo katika eneo lililotengwa kwa ajili ya familia za wahanga, watu waliojeruhiwa wakati huo na mashahidi wa mashambulizi hayo.

Sherehe ya Jumapili hii, iliyoandaliwa na manispaa ya mji wa Paris, inatamatisha wiki ya rambirambi kwa waathirika wa mashambulizi ya mwezi Januari ambapo watu 17 waliuawa na mwezi Novemba ambapo watu 130 waliangamia.

Mwanamuziki mashuhuri, Johnny Hallyday, ambaye amekua amevaa nguo nyeusi, ameimba muziki unaojulikana kama "Jumapili moja ya Januari," wimbo uliotungwa na Jeanne Cherhal ambaye anakaribisha hasa maandamano ya Januari 11, 2015 ambayo yaliwaleta pamoja zaidi ya watu milioni moja na viongozi wengi wa kigeni mjini Paris.

Chaguo la mwanamuziki wa Rock limepingwa na kundi la washirika wa karibu wa mchoraji wa katuni wa gazeti la kila wiki la Charlie Hebdo aliyeuawa katika mashambulizi ya mwezi Januari lakini chaguo hilo limetetewa na manispa ya mji wa Paris kama muimbaji maarufu na kuwa wimbo huo umetungwa vizuri kwa "tafakari" ya matukio hayo.

Rais Hollande ameweka shada la maua kwenye eneo la Jamhuri. Kisha, sherehe ilipofikia tamati, alitembelea kwa kushtukiza Msikiti Mkuu wa mji wa Paris, ambako "alikutana kwa mazungumzo na viongozi wa jamii ya Waislamu nchini Ufaransa, Ikulu ya Elysée, imearifu. Akipokelewa na kiongozi wa Msikiti, Daliyl Boubaker, na mwenyekiti wa Baraza la Waislamu nchini Ufaransa (CFCM), Anwar Kbibech, Rais Hollande na Waziri wa Mambo ya Ndani Bernard Cazeneuve wamezungumza kwa muda wa nusu saa na viongozi hao wa jamii ya Waislamu nchini Ufaransa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana