Pata taarifa kuu
UFARANSA-UISLAM-UGAIDI

Cazeneuve aomba "Waislamu wa Ufaransa kuwajibika"

Serikali ya Ufaransa imewataka Waislam nchini humo kuwajibika katika kudumisha amani na usalama.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, Januari 7, 2016 jijini Paris.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, Januari 7, 2016 jijini Paris. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Jamhuri inahitaji zaidi Waislamu wote wa Ufaransa kuwajibika", Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, ametangaza Jumamosi hii, alipoalikwa kuchangia "chai ya udugu" katika Msikiti wa St-Ouen (Val-d'oise), wakati wa kikao kilichowakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka dini ya Uislam nchini Ufaransa, ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali.

Nchini kote Ufaransa, Jumamosi na Jumapili, kwa wito wa Baraza Kuu la Waislam nchini Ufaransa (CFCM), Misikiti imetakiwa kufungulia milango wananchi wote ili kubadilishana fikra na kuchangia "chai ya udugu."

Waziri wa mambo ya ndani amekaribisha "mwelekeo huo wenye ishara inayoonyesha jinsi gani wananchi wanatakiwa kuishi pamoja nchini Ufaransa", katika mazingira magumu kwa Waislamu, ambao mara nyingi wametengwa tangu mashambulizi ya mwezi Januari na Novemba 2015.

"Wakati wimbi la ghasia linawakumba vijana bila kujali dini, watu wa kwanza kuteseka katika suala nzima la uharibifu wa dini yao ni Waislamu, ambao wana upendo wa dhati kwa taifa la Ufaransa", amekumbusha Waziri Cazeneuve, akiongeza kuwa nchi "haijidanganyi" na "haikatai kuwa hali yoyote ambayo inaweza ikatokea".

"Kutoakana na tishio kubwa la ugaidi linaloendelea kuikumba Ufaransa na baadhi ya nchi duniani, tunahitaji zaidi ulinzi wa taifa, kwa watoto wote wa Ufaransa", Waziri Cazeneuve ameongeza.

Msikiti wa St-Ouen una miezi minane tu tangu ufunguliwe, baada ya miaka kadhaa jamii ya Waislamu wakisubiri mahali pakufanyia ibada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.