Pata taarifa kuu
MASHAMBULIZI YA PARIS-FRANCE-MAREKANI-SYRIA-IS

Washington yatangaza kifo cha mshirika wa karibu wa Abaaoud

Raia wa Ufaransa Charafe El Mouden, mpiganaji wa kundi la Islamic State aliyehusika moja kwa moja katika mashambulizi ya jijini Paris, kwa mujibu wa Jeshi la Marekani, ameuawa nchini Syria wakati wa mashambulizi ambayo pia yamewaua wapiganaji wengine muhimu kadhaa wa kundi hilo.

Charaffe El Mouden, mpiganaji wa kiislamu, raia wa Ufaransa aliyeuawa nchini Syria Desemba 2015.
Charaffe El Mouden, mpiganaji wa kiislamu, raia wa Ufaransa aliyeuawa nchini Syria Desemba 2015. AFP
Matangazo ya kibiashara

El Mouadan alikuwa akishirikiana "moja kwa moja" na mwanamgambo wa kiislamu kutoka Ubelgiji, Abdelhamid Abaaoud, na "alikua akiandaa mashambulizi mengine katika nchi za Magharibi" amesema afida wa jeshi la Marekani, Kanali Steve Warren, msemaji wa muungano unaopambana dhidi ya kundi la Islamic StateEI, akifafanua kifo cha cha raia huyo wa Ufaransa.

Hata hivyo, wachunguzi wa Ufaransa wameonekana kuwa makini kufuatia taarifa hiyo. "Kwa sasa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuhusika kwake" katika mashambulizi ya Novemba 13 yaliyosababisha vifo vya watu 130 na mia kadhaa kujeruhiwa, chanzo kilio karibu na kesi hiyo kimeliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Hata hivyo, chanzo hicho kimebaini kwamba El Mouadan alikuwa mshirika wa karibu na moja wa washambuliaji waliojitoa mhanga katika ukumbi wa maonyesho wa Bataclan, Samy Amimour, na kimesema kumtambua mwingine, Omar Ismail Mostefai.

Chanzo cha kupambana na ugaidi pia kimesema kuwa hakikujua kuwa kulikuwepo na uhusiano wa El Mouadan na Abaaoud.

Kwa mujibu wa Kanali Warren, mpiganaji mwingine wa kundi la IS ambaye alikuwa na "uhusiano na mtandao uliohusika katika mashambulizi ya mjini Paris" aliuawa Desemba 26, siku mbili baada El Mouadan.

Hakim Abdel Kader alikuwa mpiganaji mashuhuri na mtaalam katika wa kugushi nyaraka, jeshi la Marekani limeeleza. Afisa huyo wa jeshi la Marekani hakutoa maelezo zaidi na wachunguzi wa Ufaransa wameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa hawamjui.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.