Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Waasi wanane wa Kikurdi wauawa kusini mashariki mwa Uturuki

media Uharibifu katika mji wa Silvan, kusini mashariki mwa Uturuki baada ya mapigano kati ya polisi ya Uturuki na wanachama PKK, Septemba 12, 2015. AFP/AFP/

Waasi wanane wa kundi la waasi cha (PKK) wameuawa na vikosi vya usalama kusini mashariki mwa Uturuki, ambapo operesheni kabambe inaendelea, uongozi wa kijeshi umesema Jumatano hii.

Waasi hao wa Kikurdi kutoka Uturuki "walidhibitiwa" Jumanne hii katika eneo la Cizre, katika mkoa wa Sirnak (kusini mashariki), uongozi wa jeshi umesema katika taarifa uliorusha kwenye tovuti yake.

Idadi kubwa ya wanajeshi - 10,000, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki - na vikosi maalum vya polisi vilivamia miji kadhaa kusini mashariki inayokaliwa na raia wengi kutoka jamii ya Wakurdi wa Uturuki, iliyowekwa chini ya amri ya kutotoka nje, ikiwa ni pamoja miji ya Cizre, Silopi, Diyarbakir, Nusaybin na Dargeçit.

Mapigano makali yalitokea kati ya vijana wafuasi wa PKK na yalienea katika maeneo karibu yote yanayokaliwa na watu kutoka jamii ya Wakurdi na kusababisha maeneo yote kukumbwa na vita.

Wakihojiwa Jumatano asubuhi kwa njia ya simu na shirika la habari la Ufaransa la AFP, wakazi wa Silopi na Cizre wamearifu uwepo wa magari ya kivita ya jeshi na kubaini kwamba kumetokea milipuko ya mabomu.

Mbunge wa chama cha HDP, kinachounga mkono Wakurdi), Ferhat Encu amerusha kwenye akaunti yake ya Twitter picha ya askari wakisukuma mlango wa jengo ambamo alikuemo katika mji wa Silopi.

"Wako wanafanya uharibifu. (...) Wanajaribu kuvunja nia ya raia. Lakini ujasiri wa Wakurdi, ambao uko sawa kwa karne kadhaa, utashinda tishio hili", Encu amesema kwa vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa shirika la habari linalounga mkono Wakurdi, FIRAT NEWS, mtoto 1 mwenye umri wa miaka 11 ameuawa wakati wa operesheni ya jeshi katika mji wa Cizre. Habari hii haijathibitishwa rasmi.

Baada ya zaidi ya miaka miwili ya usitishwaji vita, mapigano makali yalianza upya katika majira ya joto yaliyopita kati ya askari polisi na wanajeshi wa Uturuki na PKK, na kusababisha vifo vya watu wengi. askari polisi watatu waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa Jumanne hii katika eneo la Silvan katika shambulio la bomu lililohusishwa kundi la PKK, shambulio ambalo lililenga gari ya kivita.

Siku moja kabla, waandamanaji wawili vijanawaliuawa kwa risasi wakati wa makabiliano na polisi wakati ambapo wamekua wakishtumu amri ya kutotoka nje iliyowekwa tangu Desemba 2 katika wilaya ya Sur katika mkoa wa Diyarbakir.

Katika kutangaza ushindi wa chama chake katika uchaguzi wa bunge wa Novemba 1, Rais Recep Tayyip Erdogan alisema nia yake ya "kulitokomeza" kundi la PKK.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana