Pata taarifa kuu
UHISPANIA-SIASA-SHERIA

Uhispania: Mahakama ya Katiba yafuta azimio la Bunge la Catalonia

Mahakama ya Katiba nchi Uhispania imefuta Jumatano hii azimio la Bunge la Catalonia, ambalo lilianzisha rasmi mchakato wa uhuru katika jimbo la Catalonia, lakini serikali ya mkoa huo mara moja imefahamisha kuwa uamuzi huo ni batili.

Rais jimbo linalotaka kujitenga la Catalonia Artur Mas, wakati wa kikao cha Bunge katika mji wa Barcelona, Novemba 9, 2015.
Rais jimbo linalotaka kujitenga la Catalonia Artur Mas, wakati wa kikao cha Bunge katika mji wa Barcelona, Novemba 9, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Azimio hili "linakiuka viwango vya kikatiba ambavyo vinawapa watu wa Uhispania uhuru wa taifa", Mahakama imesema.

Majaji wamesisitiza kuwa Bunge Catalonia haliwezi "kujipa uhalali wa majukumu ya sheria na siasa, hadi kujipa uwezo wa kukiuka utaratibu wa kikatiba".

Majaji kumi na mbili wamechukua uamzi wao kwa "kauli moja", kiongozi wa serikali ya kihafidhina Mariano Rajoy amesema, huku akijipongeza.

Uamuzi huo unakuja zikisalia wiki tatu kabla ya uchaguzi wa wabunge na siku moja kabla ya ufunguzi rasmi wa kampeni za uchaguzi (Alhamisi usiku wa manane). Bw. Rajoy anawania muhula mwingine wa miaka minne na anadai kuwa ni msimamzi wa "umoja usio kuwa na mwisho" wa Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.