Pata taarifa kuu
TABIA NCHI-UFARANSA-UFUNGUZI

COP21: changamoto za mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

Jumatatu hii Novemba 30, marais na viongozi wa serikali 150 wanatazamiwa kukutana katika mji wa Bourget, karibu na mji wa Paris, ili kufungua mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (COP21).

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, Rais wa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (COP21), katika mji wa Bourget, wakati wa kikao kifupi cha kazi, Jumapili, Novemba 29, pamoja na wajumbe wanaoshiriki katika mkutano huo.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, Rais wa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (COP21), katika mji wa Bourget, wakati wa kikao kifupi cha kazi, Jumapili, Novemba 29, pamoja na wajumbe wanaoshiriki katika mkutano huo. REUTERS/Jacky Naegelen
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa viongozi hao, ni pamoja na Rais wa Marekani, Barack Obama, wa China Xi Jinping na wa Urusi Vladimir Putin. Kwa jumla, nchi marais na viongozi wa serikali kutoka nchi 195 wanakutana kuanzia Jumatatu hii hadi Desemba 11, kwa lengo kuu: kuzuia ongezeko joto duniani hadi kwenye kiwango cha digrii 2 ifikapo mwaka 2100. Lakini kuna masuala mengine na mazungumzo ambavyo vinaonekana kutokua rahisi.

"Hatujakutana mjini Paris kwa mazungumzo ya ana kwa ana, tumekutana ili kuchukua maamuzi muhimu ya kisheria", Laurent Fabius, Waziri wa mamambo ya nje wa Ufaransa na Rais wa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (COP21), amesema.

John Kerry, mwenzake wa Marekani, anapinga wazo la kulazimishwa, lakini muhimu. Anajua kwamba makubaliano ya kisheria kamwe hayatopigiwa kura na Baraza la Seneti ambalo linaundwa na idadi kubwa ya Maseneta kutoka chama cha Republican. Hata hivyo ni njia pekee ya kuhakikisha kwamba nchi zinazosambaza zaidi gesi chafu zinatekeleza ahadi zao.

Suala jingine muhimu katika mazungumzo hayo ni uanzishwaji wa utaratibu wa mapitio ya ahadi kila baada ya miaka mitano. Hatua muhimu imefikiwa, mwezi mmoja uliyopita, wakati China, ambayo bado inasita, iliunga mkono. Lakini maudhui ya utaratibu huo na kalenda yake bado havijawekwa sawa.

Mazungumzo yanaonekana kutokuwa rahisi, lakini hakuna kiongozi yeyote anayeshiriki mazungumzo hayo anayependelea kurudi katika hali iliyotokea wakati wa mkutano kama huo mjini Copenhagen, miaka sita iliyopita.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.