Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Heshima ya mwisho ya kitaifa kwa waathirika wa mashambulizi

Wiki mbili baada ya mashambulizi ya Novemba 13 nchini Ufaransa, heshima ya mwisho ya kitaifa kwa watu waliouawa katika mashambulizi hayo itafanyika Ijumaa hii Novemba 27, 2015 mjini Paris.

Eneo la Invalides jijini Paris, ambapo kutafanyika sherehe za kutoa heshima ya mwisho kwa waathirika wa mashambulizi ya Novemba 13.
Eneo la Invalides jijini Paris, ambapo kutafanyika sherehe za kutoa heshima ya mwisho kwa waathirika wa mashambulizi ya Novemba 13. Wikimedia Commons / Daniel Vorndran / DXR
Matangazo ya kibiashara

Sherehe itafanyika katika eneo la Invalides, na katika kaburi la Napoleon wa kwanza, familia za wahanga na baadhi ya watu 350 waliojeruhiwa watahudhuria sherehe hiyo.

Pembezoni mwa Rais, kutakuepo na wajumbe wote wa serikali na wawakilishi wakuu ya vyama mbalimbali vya kisiasa. heshima hii ya mwisho kwa waathirika ni ya "kitaifa na kijamhuri."

Rais wa Ufaransa François Hollande leo Ijumaa atangoza misa ya kuwakumbuka watu 130 waliouawa baada ya kushambuliwa na magaidi wa Islamic State jijini Paris.

Rais Hollande anatarajiwa kuhutubia kwa muda wa dakika 20 katika hafla hiyo ya muda wa saa moja.

Rais François Hollande, amesema kuwa anafikiri kwa hotuba yake na kwa maandalizi. Ikulu ya Elysée ilitaka sherehe rahisi katika mahali patakatifu kwa heshima ya waathirika wa mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris. Sherehe itafanyika katika ukumbi wa Invalides, eneo la kijeshi katika karne ya 17 katikati mwa mji mkuu. Kamera ztakaa mbali na familia.

Hii ni mara ya kwanza sherehe kama hii inafanyika katika ukumbi wa Invalides.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.