Pata taarifa kuu
UBELG-UGAIDI-USALAMA

Ubelgiji yaapa kukabiliana na waislamu wa itikadi kali

Ubelgiji, ambapo kuliandaliwa kwa mujibu wa viongozi wa Ufaransa, mashambulizi ya jijini Paris na katika eneo la Saint-Denis, imetangaza Alhamisi wiki hii kuimarisha sheria yake dhidi ya ugaidi, pamoja na kuwaweka kizuizini wanajihadi wanaorudi kutoka Syria na kuvunjwa kwa misikiti isiyotambuliwa na serikali.

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel, akizungumza katika Baraza la Wawakilishi, amesema kuwa watuhumiwa wa jihadi wanaorudi kutoka Syria  watakamatwa na misikiti isiyotambuliwa na serikali itavunjwa.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel, akizungumza katika Baraza la Wawakilishi, amesema kuwa watuhumiwa wa jihadi wanaorudi kutoka Syria watakamatwa na misikiti isiyotambuliwa na serikali itavunjwa. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

"Wanajihadi ambao hurudi, nafasi zao ni jela", amesema Waziri Mkuu, Charles Michel.

waziri mkuu, ambaye ameeleza kwa kina hatua hizo mbele ya Baraza la Wawakilishi, pia amebaini kuwa zaidi Euro milioni 400 zaziada zitatengwa kwa mapambano dhidi ya vurugu za kijihadi. Pesa hizo zimo katika bajeti ya mwaka 2016.

Miongoni mwa hatua nyingine zilizotangazwa, polisi wa Ubelgiji sasa wameruhusiwa kuendesha msako katika mzunguko wa saa 24 ( operesheni hiyo inmekatazwa kuendeshwa usiku kati ya 3:00 hadi saa 11:00) na kadi za simu hazitauzwa kwa mtu yeyote bila kusajiliwa.

Aidha, sheria itajadiliwa upya ili kurahisisha kupigwa marufuku, kutoa hukumu au kufukuzwa kwa wahubiri wa dini wanaotuhumiwa kueneza matamshi ya chuki.

Lakini waziri mkuu pia alitetea Idara ya Ujasusi ya nchi yake, ambayo inanyooshewa kidole tangu uchunguzi wa mashambulizi yaliyogharimu maisha ya zaidi ya watu 129 jijini Paris Ijumaa iliyopita kubaini kuwa wengi wa waliohusika katika mashambulizi hayo waliishi Ubelgiji au ni walizaliwa nchini Ubelgiji.

"Vitendo vya kivita vya Ijumaa viliamuliwa na kupangwa nchini Syria, vikaandaliwa Ubelgiji, na kutekelezwa katika ardhi yetu kwa ushirikiano na raia wa Ufaransa", François Hollande alisema Jumatatu mbele ya wabunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.