Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 07/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Taarifa za wahusika wa mashambulizi ya Paris zawekwa wazi

media Mwanajeshi wa Ufaransa akipiga doria pembezoni mwa eneo la Eiffel jijini Paris,Novemba 15, 2015. AFP PHOTO / FRANCOIS GUILLOT

Siku tano baada ya mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 13 mwezi huu mjini Paris, taarifa za wahisika wa mashambulizi hayo yameanza kuwekwa wazi huku baadhi ya nchi wakichukua taadhari kwa ajili ya usalama wao.

Taarifa hizo zimebainisha kuwa magaidi hao ni wengi kuliko ilivyokua inadhaniwa awali wakijipanga katika makundi matatu yaliyoratibiwa na uongozi wao ulioko nchini Syria ambapo saba miongoni mwao wamekamatwa pamoja na washirika wao kadhaa, mmoja au wawili wakiwa hawajashikwa bado.

Mshukiwa mkuu wa mashambulizi hayo raia wa Ubelgiji Abdelhamid Abaaoud bado haijajulikana aliko baada ya operesheni ya polisi ya Jumatano wiki hii eneo la Saint-Denis huku serikali ya Ufaransa ikiwasilisha Bungeni mswada wa sheria dhidi ya Ugaidi unaotarajiwa kupigiwa kura leo Alhamisi na wabunge wa nchi hiyo..

Sanjari na hayo, Jumatano hii Urusi imewasilisha mswada kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu azma ya pamoja ya kupambana na ugaidi wakati Ufaransa nao wakiendelea kuboresha mswada wao baada ya mashambulizi ya mjini Paris, imetangazwa na mabalozi wa nchi hizi mbili kwenye Umoja huo.

Wakati hayo yakijiri, Italia imeimarisha usalama kwenye maeneo ya kihistoria mjini Roma, Vatican na Milan baada ya kuonywa na shirika la ujasusi la Marekani FBI kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi nchini humo, ikiwa ni pamoja na eneo la makao makuu ya kanisa katoliki Mtakatifu Petro, Kanisa Kuu la mjini Milan na eneo maarufu la mji huo La Scala.

Shirika la kimataifa la ushirikiano wa polisi Interpol imebainisha idadi ya wanajihadi 5800 wa kigeni miongoni mwa makadirio ya 25,000 ambao walijiunga na makundi ya kigaidi katika nchi kama vile Syria au Iraq, wakiwemo wahusika wa mashambulizi yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 129 Novemba 13 mjini Paris.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana