Pata taarifa kuu
EU-UKAGUZI-USALAMA

Mawaziri wa mambo ya ndani wa eneo la Schengen wakutana Ijumaa

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya watakubaliana kuimarisha uchunguzi na ukaguzi wa utambulisho katika mipaka ya nje ya eneo la nchi za Ulaya zinazotumia viza ya Schengen, kwa mujibu wa rasimu ya hitimisho ambayo Reuters imeweza kusoma.

Kwenye mpaka kati ya Slovenia, mwanachama wa eneo la Schengen, na Croatia. Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulayawanatazamiwa kukutana IJumaa Novemba 20 jijini Brussel.
Kwenye mpaka kati ya Slovenia, mwanachama wa eneo la Schengen, na Croatia. Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulayawanatazamiwa kukutana IJumaa Novemba 20 jijini Brussel. REUTERS/Srdjan Zivulovic
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao watakubaliana katika mkutano wao wa siku ya Ijumaa wiki hii kwa "kutekeleza mara moja ukaguzi muhimu wenye utaratibu na kudhibiti mipaka ya nje, ikiwa ni pamoja na watu binafsi ambao wana haki ya uhuru wa kutembea", ndivyo ilivyoandikwa katika makubaliano ya rasimu ambayo yanajibu madai ya Ufaransa, iliyokumbwa na mfululizo wa mashambulizi yaliogharimu maisha ya zaidi ya watu 129 Ijumaa iliyopita mjini Paris na katika eneo la Saint-Denis, nchini Ufaransa.

Eneo la Schengen linaundwa na nchi 26, ikiwa ni pamoja na zaidi ya nchi nyingi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, isipokuwa Uingereza, Ireland, Croatia, Romania, Bulgaria na Cyprus.

Kwa sasa, Maafisa wa Idara ya forodha wamekua wakiridhika kwa kufanya ukaguzi rahisi wa pasipoti za raia kutoka Ulaya wakati raia hawa wanapoingia au kuondoka eneo la Schengen. Utaratibu mpya utahusisha vyeti vya kusafiria cheti au vyeti vya vyombo vya sheria au vyombo vya usalama.

Udhibiti huu wa mipaka ya nje ya eneo la Schengen utaanza kutekelezwa mwezi Machi 2016na kutakuwepo moja kwa moja na ukaguzi wa nyaraka za kusafiria ".

Mawaziri wa mambo ya ndani pia watakubaliana juu ya ukaguzi thabiti wa mipaka ya nje inayokabiliwa zaidi na hali ya hatari "kutokana na kupelekwa kwa Timu za kuingilia kati haraka mipakani ("Rabit ) pamoja na polisi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.