Pata taarifa kuu
URUSI-UFARANSA-SYRIA-IS-MASHAMBULIZI-USALAMA

Syria: Raqqa yakabiliwa na mashambulizi ya Ufaransa na Urusi

Raqqa, mji mkuu halisia wa kundi la Islamic State (IS) nchini Syria umeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya ndege za majeshi ya Ufaransa na Urusi.

Video iliyorushwa hewani Novemba 17, 2015 na jeshi la Ulinzi la Ufaransa ikionyesha jinsi jeshi la Ufaransa likiendesha mashambulizi katika ngome za kundi la Islamic State mjini Raqqa.
Video iliyorushwa hewani Novemba 17, 2015 na jeshi la Ulinzi la Ufaransa ikionyesha jinsi jeshi la Ufaransa likiendesha mashambulizi katika ngome za kundi la Islamic State mjini Raqqa. /ECPAD / EMA/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo tayari yamesababisha vifo vya wapiganaji 33 na kuzilazimisha familia za wapiganaji wa kigeni wa kundi hilo kukimbilia katika maeneo jirani.

Nchi hizi mbili zinataka kuendesha mashambulizi dhidi ya EI, hasa katika mji wa Raqqa, mji unaopatikana kwenye eneo la makutanio ya barabara za kaskazini mwa Syria na kudhibitiwa na kundi la Islamic State mapema mwaka 2014.

"Hapo ni mahali ambapo tupaswa kushambulia kundi la IS ", waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, alisema Jumanne wiki hii.

Kwa mujibu wa tathmini ya awali, mashambulizi ya anga ya Ufaransa na Urusi dhidi ya ghala za silaha, kambi na vituo vya ukaguzi katika mji wa Raqqa viunga vyake "yamesababisha vifo vya watu 33 na wengine wengi kujeruhiwa katika safu ya kundi la Islamic State, katika masaa 72", Rami Abdel Rahman, mkuu wa Shirika la Haki za Binadamu nchini (OSDH) ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Idadi hii ndogo ya wapiganaji waliouawa inaelezwa kwamba ni kutokana na kuwa wapiganaji wa kundi la IS walikua amechukua tahadhari tangu mapema", amesema Rami Abdel Rahmane. "Kulikuwa na walinzi tu pembezoni mwa ghala za silaha na katika kambi na wapiganaji wengi waliuawa kwenye vituo vya ukaguzi."

Familia nyingi za wapiganaji wa kigeni zimeondoka katika mji huo na kukimbilia katika mji wa Mosul, "mji mkuu" wa kundi la Islamic State nchini Iraq, ambapo ni "salama".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.