Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA-SHAMBULIO

Operesheni ya polisi pembezoni mwa mji wa Paris baada ya mashambulizi

Polisi imeendesha operesheni Jumatano wiki hii kwenye ghorofa moja katika eneo la Saint-Denis, Kaskazini mwa mji wa Paris.

Operesheni ya polisi inayopambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Saint-Denis, inayohusiana na mashambulizi ya liotokea jijini Paris, Novemba 18, 2015.
Operesheni ya polisi inayopambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Saint-Denis, inayohusiana na mashambulizi ya liotokea jijini Paris, Novemba 18, 2015. LIONEL BONAVENTURE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii imekua ikimlenga mshukiwa wa maandalizi ya mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu wengi Novemba 13, ambapo hatima yake bado haijulikani, katika operesheni iliyosababnisha vifo vya watu waili, ikiwa ni pamoja na mshambuliaji mwanamkealiyejitoa mhanga.

Watu saba wamekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wakati wa operesheni hiyo ya polisi, ambayo yalisababisha urushianaji risasi kati ya polisi na watu wenye silaha, ikiwa ni pamoja na mshambuliaji mwanamke aliyejitoa mhanga, akiwa ni mwanamke wa kwanza nchini Ufaransa.

Akizungumza baada ya operesheni hiyo, François Hollande ametoa wito kwa raia wa Ufaransa kuwa "wajasiri" na kutokua na "hofu", baada ya mauaji yaliotekelezwa na kundi la Islamic State (IS) katika mji wa Paris, "ambalo linataka kukuza chuki", "unyanyapaa" na kusababisha "mgawanyiko".

Ukaguzi unaendelea ili kujua kama mwajihadi kutoka Ubelgiji, Abdelhamid Abaaoud, jina la utani Abu Omar al-Baljiki (Mbeleji), anayetuhumiwa kuwa mwanzilishi au mratibu wa mashambulizi yaliosababisha vifo vya zaidi ya watu 129 jijini Paris na pembezoni mwa Uwanja wa taifa wa michezo (Stade de France) katika eneo la Saint-Denis, alikua katika ghorofa iliolengwa.

Wakati wa operesheni hiyo iliyoanza alianza Jumatano alfajiri na kumalizika mapema asubuhi, katikati ya eneo la Saint-Denis lilikua limezingirwa, wakazi 15,000 hadi 20,000 wa eneo hilo walitakiwa kukaa nyumbani.

Hata hivyo askari polisi sita wamejeruhiwa katika operesheni hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.