Pata taarifa kuu
UFARANSA-SYRIA-MASHAMBULIZI-USALAMA

Ufaransa yajibu na kushambulia ngome za kundi la IS Syria

Ufaransa imeendesha mashambulizi makubwa Jumapili Novemba 15 dhidi ya ngome za kundi la Islamic State katika eneo linalolidhibiti la Raqqa nchini Syria. Hii ni operesheni kubwa iliyofanywa na Ufaransa tangu ilipanza kuingilia kati kijeshi nchini Syria mwezi Septemba mwaka jana.

Picha ya ndege za kivita aina ya Rafale, iliyorushwa hewani na idara ya wizara ya ulinzi ya Ufaransa wakati jesh la Ufaransa lililopoanza kuingilia kati nchini Syria mwezi Septemba uliopita.
Picha ya ndege za kivita aina ya Rafale, iliyorushwa hewani na idara ya wizara ya ulinzi ya Ufaransa wakati jesh la Ufaransa lililopoanza kuingilia kati nchini Syria mwezi Septemba uliopita. AFP PHOTO / ECPAD
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Anga la Ufaransa limeendesha mashambulizi makubwa Jumapili hii usiku katika jimbo la Raqqa. Ndege kumi na mbili zimeshiriki katik aoperesheni hiyo, ikiwa ni pamoja na ndege za kivita kumi. Ni jumla ya karibu ndege zote za kivita zilizopo katika kambi ya jeshi la Ufaransa katika Umoja wa Falme za Kiarabu na katika kambi nyingine iliopo Jordan, ambapo Ufaransa ina ndege kumi na mbili za kijeshi aina ya Rafale na Mirage 2000.

Mashambulizi hayo yameendeshwa mara mbili kwa tafauti ya saa moja na nusu, wizara ya ulinzi ya Ufaransa imesema. Shambulio la kwanza, lililondeshwa saa 1:50 usiku, lililenga eneo muhimu ambapo kunapatikana "makao makuu ya kundi la Islamic, kituo wanakosajili wapiganaji wapya na ghala la silaha na vifaa vingine vya kijeshi" vya kundi Islamic State. Shambulio la pili, limeendeshwa saa 2:25 usiku ,na lililenga "kambi ya mafunzo ya kigaidi". Zaidi ya mabomu ishirini yamerushwa katika maeneo hayo wakati wa operesheni hiyo iliofanyika "kwa ushirikiano na majeshi ya Marekani."

Mashambulizi ya Ufaransa muhimu Syria

Mashambulizi haya muhimu tangu Ufaransa ilipoingilia kijeshi Syria Septemba 27, ni ya kwanza yalioahidiwa na François Hollande, masaa 48 baada ya mashambulizi mjini Paris.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian amezungumza Jumapili kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani, Ashton Carter. Kwa mujibu wa Pentagon, Paris na Washington wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao na kufanya operesheni endelevu dhidi yakundi la Islamic State. Wamarekani wamekubali kutoa taarifa zozote. Na labda, wao ndio walitoa taarifa ya maeneo yaliolengwa Jumapili hii usiku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.