Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Mashambulizi ya Paris: Uchunguzi waendelea, washambuliaji watatu watambuliwa

Uchunguzi wa mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu wengi nchini Ufaransa umepelekea katika siku mbili kubaini watatu kati watu wa saba waliojitoa mhanga, wakati ambapo wito kwa mashahidi umetolea Jumapili Novemba 15 ili kumpata ndugu wa mmoja wao,anayechukuliwa kama "mtu hatari".

Abdeslam Salah, mwenye umri wa miaka 26 na amezailwa Ubelgiji, anatafutwa baada ya polisi ya Ufaransa kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake..
Abdeslam Salah, mwenye umri wa miaka 26 na amezailwa Ubelgiji, anatafutwa baada ya polisi ya Ufaransa kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake.. REUTERS/Police Nationale
Matangazo ya kibiashara

Katika uchunguzi: utambulisho wa watu "kutoka makundi matatu ya kigaidi", uliowekwa wazi na vyombo vya sheria, waliendesha mashambulizi Ijumaa usiku katika Uwanja wa taifa wa michezo (Stade de France), katika ukumbi wa tamasha wa Bataclan tamasha na katika baa na migahawa kadhaa mjini Paris.

Mashambulizi, ambayo yamesababisha vifo vya zaoidi ya watu 129 na 352 kujeruhiwa, yalidaia kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS).

Licha ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyetambuliwa tangu Jumamosi wiki iliopita, "magaidi wengine wawili (...) wametambuliwa rasmi leo" kwa "alama za vidole vyao", mwendesha mashitaka amesema Jumapili hii. Wote wawili wanaishi Ubelgiji na ni raia wa Ufaransa..

Mmoja, anaitwa Bilal Hadfi, mwenye umri wa miaka 30, ni moja wa washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga ambao walijilipua katika Uwanja wa taifa wa michezo (Stade de France). Mwengine, Abdeslam Brahim, mwenye umri wa miaka 31, alijilipua kwenye barabara kuu ya Voltaire, bila hata hivyo kusababisha maafa.

Abdeslam Brahim ni miongoni mwa ndugu watatu waliohusishwa katika wachunguzi: mmoja wa ndugu hao, Mohamed, aliwekwa chini ya ulinzi nchini Ubelgiji. Idara zinazopambana dhidi ya ugaidi hazina taarifa ya mtu watatu, Salah, ambaye anaweza kuwa pia mmoja wa washambuliaji wa waliojitoa mhanga au yuko mafichoni, kwa mujibu wa vyanzo vilio karibu ya faili hiyo. Vyombo vya sheria vya Ubelgiji vimetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na polisi ya Ufaransaimetoa wito kwa mashahidi dhidi ya mtu huyo "hatari".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.