Pata taarifa kuu
URUKI-UFARANSA-MASHAMBULIZI-UGAIDI-USALAMA

Ankara kuionya Ufaransa kuhusu mashambulizi ya kujitoa mhanga Paris

Uturuki imesema Jumatatu kuwa ilionya mara mbili katika mwaka mmoja Ufaransa juu ya wanamgambo wa kijihadi ambao waalijilipua Ijumaa jioni katika mashambulizi ya Paris, lakini imesikitika kuona Ufaransa haikuzingatia onyo hilo.

Sakafu ya Ukumbi wa tamasha wa Bataclan bado umefunikwa kwa ajili ya uchunguzi, Novemba 15, 2015, Paris.
Sakafu ya Ukumbi wa tamasha wa Bataclan bado umefunikwa kwa ajili ya uchunguzi, Novemba 15, 2015, Paris. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Polisi ya Uturuki ilitoa "taarifa mara mbili kwa polisi ya Ufaransa mwezi Desemba 2014 na mwezi Juni 2015", kuhusu Omar Ismail Mostefai, mmoja wa washambuliaji wa ukumbi wa tamasha wa Bataclan jijini Paris, afisa wa serikali ya Uturuki ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Hatukupata jibu kutoka serikali ya Ufaransa kuhusu suala hili", afisa wa serikali ya Uturuki ambaye hakutaka kutajwa jina amelaumu.

Mwezi Oktoba 2014, Uturuki ilipokea ombi la taarifa kutoka Ufaransa kuhusu watuhumiwa 4 wa kijihadi ambayo haikuelewa jina la mshambuliaji wa kujitoa mhanga wa Paris, chanzo hicho kimesema.

Uturuki, hata hivyo, iliendesha uchunguzi kuhusu suala hilo kwa sababu alikuwa na uhusiano na kundi linalolengwa na vyombo vya usalam vya Ufaransa, chanzo hicho kimeongeza.

Omar Ismail Mostefai alishiriki katika utekaji nyara uliosababisha vifo katika ukumbi wa tamasha wa Bataclan kabla ya kujilupua. Alitambuliwa kwa alama yake ya kidole.

Kwa mujibu wa vyombo vya Ufaransa, Omar Ismail Mostefai alihukumiwa mara kadhaa makosa mbalimbali na kwa msimamo wake mkali wa kidini tangu mwaka 2010 lakini hakuwahi kuhusika kamwe katika kesi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.