Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Kitisho na hisia duniani baada ya mashambulizi ya Paris

Mfululizo wa kipekee wa mashambulizi ya kigaidiyaliosababisha vifo vya watu 20 katika mji wa Paris Ijumaa usiku wiki hii yamesababisha wimbi la hofu na hisia duniani kote.

Rais Barack Obama katika taarifa kuhusu mashambulizi katika mji wa Paris Novemba 13, 2015 katika Ikulu ya White House mjini Washington.
Rais Barack Obama katika taarifa kuhusu mashambulizi katika mji wa Paris Novemba 13, 2015 katika Ikulu ya White House mjini Washington. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutoka Washington na Moscow, Umoja wa Mataifa hadi NATO, kote Ulaya, viongozi wa wamelaani mauaji hayo, ambayo pia yamesababisha zaidi ya watu 200 kujeruhiwa, 80 wakiwa katika hali mbaya, na wameihakikishia Ufaransa uchungu walio nao, mshikamano na msaada kwa raia wa Ufaransa na taifa hilo.

Katibu Mkuu wa Umoj awa Matiafa Ban Ki-moon amelaani kwa mujibu wa msemaji wake "mashambulizi ya kigaidi ya kijinga" na kusema "wako pamoja na serikali na raia wa Ufaransa."

Katika taarifa ya pamoja, nchi kumi na tano wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matiafa "wamelaani suala mashambulizi na vitendo vya kigaidi" vilipendeshwa katika mji wa Paris.

Mashambulizi haya "si tu mashambulizi dhidi ya mji wa Paris" lakini "mashambulizi dhidi ya binadamu wote na maadili yetu kwa pamoja", Rais wa Marekani Barack Obama amesema wakati wa hotuba yake katika Ikulu ya White House.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry katika taarifa yake, amesema "vitendo vya kutisha na na vya kuchukiza" ambavyo ni "shambulio dhidi ya raia wetu wa pamoja."

Urusi, ambayo ambayo imelaania "mauaji ya kinyama", amesema iko tayari kutoa "msaada wowote katika uchunguzi wa uhalifu wa kigaidi."

Rais Vladimir Putin ametoa rambirambi zake na mshikamano kutoka Urusi kwa Rais François Hollande na raia wa Ufaransa, kwa mujibu wa shirika la habari la TASS.

Mjini Tehran, Rais Hassan Rouhani, ambaye ameahirisha ziara yake iliyotarajiwa barani Ulaya baada ya mashambulizi, amelaani mashambulizi hayo, na kuyaita "uhalifu dhidi ya ubinadamu".

Wasiwasi na hasira

China imesema "kushtushwa na mashambulizi hayo". "Ugaidi ni adui wa wanadamu wote. Chinainaunga mkono Ufaransa katika jitihada zake za kuleta amani na utulivu na kupambana na ugaidi", Beijing imeongeza.

Japan pia imesema "kushtushwa" na mashambulizi hayo, baada ya "vitendo hivyo vya kigaidi na unyama vya kutisha" na serikali yake imejikubalisha kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa "kuzuia ugaidi".

Rais wa Tume ya Ulaya , Jean-Claude Juncker, katika Twitter, ameelezea "wasiwasi" wake, kuhu akielezea "mshikamano kamili na watu wa Ufaransa".

"Ufaransa iko katika mstari wa kwanza katika mapambano dhidi ya ugaidi. Lakini haiko pekee yake. Mapambano haya ni vita ya raia wote wa Ulaya, na watu wote duniani kuwa huru", amesema kwa upande wake Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk.

"Ugaidi kamwe hautohinda demokrasia", amesema pia Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, huku akisema kutiwa wasiwasi na mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.