Pata taarifa kuu
FIFA-BLATTER-PLATINI-SOKA

Sepp Blatter adai kuwa bado ni rais wa FIFA

Akiwa amesimamishwa kwa muda kwenye nafasi ya rais wa Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA), Sepp Blatter, ameendelea kupumzika katika hospitali alikokuwa amelazwa Ijumaa iliyopita na anatazamiwa kuondoka haraka iwezekanavyo, mmoja wa washirika wake wa karibu amesema Jumatano hii.

Sepp Blatter ameliongoza Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kipindi cha miaka 17.
Sepp Blatter ameliongoza Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kipindi cha miaka 17. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Stöhlker Klaus ameiambia shirika la habari la Uingereza la Reuters kwamba Sepp Blatter, ambaye ana umri wa miaka 79, bado anachukuliwa kama rais wa FIFA licha ya kusimamishwa kwa muda wa siku 90, uamzi uliochukuliwa dhidi yake na kamati ya maadili ya taasisi hiyo.

"Nadhani hali yake binafsi ni nzuri, anapumzika kwa siku kadhaa na kisha nadhani mwishoni mwa wiki au siku ya Jumatatu (ataondoka hospitalini)", Klaus Stöhlker amearifu. "Wakati nilimwita leo asubuhi katika hospitali hiyo, tulizungumza vizuri (...), alionekana akiwa imara, amesema ubongo na moyo wake vinaendelea vizuri".

Sepp Blatter amelazwa hospitali tangu siku ambapo mwanasheria wake, raia wa Marekani, Richard Cullen alitoa taarifa ikionyesha kuwa rais wa FIFA aliruhusiwa kulazwa hospitalini kwa ajali ya uchunguzi wa afya yake. Klaus Stöhlker ameeleza kuwa Sepp Blatter alikuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo wakati wa maandamano yaliofanyika katika mji alikozaliwa wa Valais, na aliona kuwa "mwili wake haukuwa unafanya kazi kama ilivyo kuwa."

Sepp Blatter, rais wa FIFA tangu mwaka 1998, na Rais wa shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA), Michel Platini, ambaye alipewa nafasi kubwa ya kumrithi kiongozi huyo wa FIFA Februari 26, walisimamishwa Oktoba 8 na Tume ya Maadili ya FIFA kwa sababu ya mashaka juu ya uhalali wa malipo ya Euro milioni 1.8 zilizolipwa mwaka 2011 na Blatter kwa Platini. Alipigwa marufugu kwenda kwenye makao makuu ya FIFA mjini Zurich na katika viwanja vya michezo zinakochezwa mechi za kandanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.