Pata taarifa kuu

Wahamiaji milioni 3 wanatazamiwa kuwasili Ulaya ifikapo 2017

Hali ya hatari kwa wahamiaji imeshuhudia Alhamisi hii katika Bahari ya Aegean ambapo watoto wawili wamekufa maji, na kusababisha hali ya hatari katika kisiwa cha Lesbos. 

Wahamiaji katika mji wa Slovenia wa Šentilj, kwenye mpaka na Austria, Novemba 4, 2015.
Wahamiaji katika mji wa Slovenia wa Šentilj, kwenye mpaka na Austria, Novemba 4, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji wanataka tatizo la kufa maji likomeshwe mara moja kati ya Uturuki na Ugiriki, eneo ambalo litaendelea kushuhudia hali ya taharuki kufuatia wahamiaji 600,000 wapya wanaotarajiwa kuwasili ifikapo mwezi Februari.

Tume ya Ulaya kwa upande wake imesema Alhamisi hii katika utabiri wake wa kiuchumi kwamba wahamiaji milioni tatu wanatarajiwa kuwasili barani Ulaya ifikapo mwaka 2017, na kusababisha "athari" lakini chanya katika ukuaji wa uchumi.

Kwa sasa, ni hali mbaya ya kibinadamu ambayo imeendelea kuongeza: watoto wawili ikiwa ni pamoja na msichana mdogo na mvulana wamekufa maji usiku wa Jumatato kuamkia Alhamisi wiki hiibaada ya meli yao kuzama, katika pwani ya kisiwa cha Kos, katika mfereji unaosafirisha maji nchini Uturuki . Hali mbaya ya hewa katika eneo hilo imesababishavifo vya wahamiaji 90, wengi wao wakiwa watoto, tangu wiki iliyopita.

Mwili wa msichana huyo mdogo umepatikana, wakati ambapo zoezi la kuutafuta mwili wa mvulana mdogo, mwenye umi wa miaka sita bado linaendelea. Baba wa mvulana huyo, ambaye ni miongoni mwa manusura 14 waliokua katika meli iliozama, amesema kuwa alijaribu kumuokoa mwanae, bila mafaanikio, na hivyo kuachana na zoezi hilo kwa kuweza kuwasaidia abiria wengine.

Kwa jumla, zaidi ya wahamiaji 752,000 na wakimbizi wamewasili barani Ulaya mwaka huu na wengine 3440 walipoteza maisha aukutoweka wakati wa kuvuka bahari ya Mediterranean, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Matifa linalohudumia wakimbizi HCR. Zaidi yawahamiaji na wakimbizi 608,000 wamewasili nchini Ugiriki na wengine140,200 nchini Italia.

Ili kujaribu kuzuia kuvuka bahari ya Mediterranean, Umoja wa Ulaya utajaribu kupata msaada wa ziada kutoka nchi za Afrika ili kudhibiti wimbi la wahamiaji katika mkutano wa kilele wa Valletta umeopangwa kufanyika Malta tarehe 11 na 12 Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.