Pata taarifa kuu
TABIA NCHI-UFARANSA-CHINA

Tabia nchi: Hollande apata "mkataba kabambe" kutoka Beijing

Jumatatu hii, Ufaransa na China wamekubaliana "kufikia makubaliano ya kisheria" katika mkutano wa Paris kuhusu hali ya hewa. Mawaziri watano, viongozi 23 wa ngazi ya juu, viongozi 50 wa makampuni... François Hollande katika ziara yake nchini China amejikita sana kwa uchumi wa Ufaransa, lakini hasa kwa suala la mabadiliko tabia nchi.

Rais wa China Xi Jinping (kushoto) akimpokea Rais wa  Ufaransa François Hollande (kulia) Kwa ziara rasmi ya siku mbili.
Rais wa China Xi Jinping (kushoto) akimpokea Rais wa Ufaransa François Hollande (kulia) Kwa ziara rasmi ya siku mbili. REUTERS/Jason Lee
Matangazo ya kibiashara

Lengo liliwekwa wazi na François Hollande alipowasili nchini China : Ufaransa inatarajia kwa mchafuzi mkubwa duniani kutoa ahadi zake kabla ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabia nchi mjini Paris. Jumatatu hii, matarajio ya Rais wa Ufaransa yamesikilizwa : China ilikubali kujitoa. Ni kuendelea na juhudi baada suala la tabia nchi, kwa kile kinachoitwa "mapitio ya mkataba". Kila baada ya miaka mitano, kunyika tathmini ya kujua kila nchi imefikia wapi na kama nchi zote zimetekeleza ahadi zao.

François Hollande anataka kuamini: utaratibu huu utawezesha juhudi zaidi. Hii ni hatua muhimu kweli, hasa wakati inapokumbukwa kuwa siku chache zilizopita, Umoja wa Mataifa alionya, pamoja na ahadi zilizopo, kinachojulikana "michango" ya nchi, wakati ambapo inajulikana kuwa kiwango cha joto duniani kimefikia kwenye 2.7 ° C, huku mashirikia yasio ya kiserikali yakisema kiwango hicho kimefikia kwenye kipimo cha 3, mbali na 2 ° C kilichoonyeshwa.

Kushindwa kwa mkutano wa Copenhagen

Kwa mujibu wa Francois Hollande, ahadi za Beijing ni mafanikio makubwa. Rais wa Ufaransa alikuwa na utaratibu huu, Jumatatu mchana: "Tuliweka masharti ya yatakayopelekea mafaniko katika mkutano wa Paris ."

Kwa upande wa wanamazingira, tayari wana wasiwasi mkubwa.Mbunge wa Umoja wa Ulaya Yannick Jadot amesema: "Utaratibu huui, si wa kisheria, hauaeleweki." Kwa kweli, wanamazingira wanakumbuka kwamba mwaka 2009 mjini Copenhagen, ni China ambayo ilichangia kufuta mkataba.

Hata hivyo huu ni wakati muhimu katika historia ya China. Lengo la Beijing leo ni kuwa kiongozi wa ulimwengu katika ukuaji wa masuala ya kijani. Serikali inataka hasa kuhakikisha msaada umeifikia jamii ya wenye maisha ya kati waishio mijini ambao wanataka maisha bora, wakati ambapo jamii hiyo inakabiliana na uchafuzi wa kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.