Pata taarifa kuu
UTURUKI-UCHAGUZI-SIASA

Chama cha AKP chapata ushindi katika uchaguzi

Chama cha Rais Recep Tayyip Erdogan kimeshinda uchaguzi wa bunge nchini Uturuki wa Jumapili na kimrfanikiwa, dhidi ya takwimu zote, kwa kupata viti vingi kiliyopteza miezi mitano iliyopita.

Wafuasi wa chama cha AKP washerehekea ushindi wa chama hicho mbele ya picha ya Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, Novemba 1, 2015, Istanbul.
Wafuasi wa chama cha AKP washerehekea ushindi wa chama hicho mbele ya picha ya Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, Novemba 1, 2015, Istanbul. UMIT BEKTAS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla ya kura zote zilizohesabiwa, chama tawala cha Sheria na Maendeleo (AKP) kimepata 49.2% ya kura na kimeshinda vita 316 kwa jumla ya viti 550, vya wabunge, runinga za NTV na CNN-Türk zimetangaza.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa kwa siku kadhaa zijazo lakini karibu kura zote zimeshahesabiwa ambapo chama hicho cha AKP kimejikusanyia zaidi ya asimilia hamsini kutawala bunge.

Matokeo hayo yatampa nguvu rais Recep Tayyip Erdogan ambaye aliita kura hiyo kama kura ya amani na ujumbe kwa wanamgambo wa kikurdi na kudai kuwa vurugu haziwezi kuishinda demokrasia.

Chama kinachoungwa mkono na Wakurdi cha HDP kimepata zaidi ya asilimia kumi zilizopigwa.

Katika eneo la kusini mwa mji wa Diyarbakir kulitokea makabiliano kati ya askari polisi na wafuasi wa chama hicho cha Kikurdi. Wandamanaji waliwatupia polisi mawe na mafataki huku polisi nao wakijibu kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Kufuatia ushindi wa chama chake cha AK Waziri mkuu wa nchi hiyo Ahmet Davutoglu ametoa hutuba ya kitamaduni katika makao makuu ya chama hicho mji Ankara. Davutoglu amesema chama chake kitaongoza kwa niaba ya Waturuki wote.

Matokeo haya yanaonekana kama tofauti kubwa kwa Erdogan, mwenye umri wa miaka 61. Juni 7, chama chake kilipoteza udhibiti wa jumla kiliyokua kikishikilia kwa kipindi cha miaka kumi na tatu kwenye Bunge, kufaulu ndoto yake ya kudhibiti "umiliki " wa moja kwa moja kwenye mamalaka ya uongozi wa nchi.

" Leo ni siku ya ushindi "
, amekaribishwa Waziri Mkuu anayemaliza muda wake na kiongozi wa chama cha AKP, Ahmet Davutoglu, katika ngome yake kuu ya Konya (katikati) mwa nchi. " Leo hii hakuna walioshindwa bali wote ni washindi ", Dutoglu ameongeza, huku akiwanyooshea mikono wapinzani wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.