Pata taarifa kuu
UTURUKI-UCHAGUZI-SIASA

Uturuki: kampeni za uchaguzi zagubikwa na vurugu

Kampeni za uchaguzi ziligubikwa na vurugu, ikiwa ni pamoja na kurudi kwa mapigano kati ya vikosi vya Uturuki na waasi wa Kikurdi wa PKK, kusini-Mashariki mwa Uturuki.

Mfuasi wa chama cha AKP wakati wa kampeni ya uchaguzi iliyoandaliwa Oktoba 29 na chama tawala katika eneo la Diyarbakir.
Mfuasi wa chama cha AKP wakati wa kampeni ya uchaguzi iliyoandaliwa Oktoba 29 na chama tawala katika eneo la Diyarbakir. REUTERS/Sertac Kayar
Matangazo ya kibiashara

Ni katika eneo hasa ambapo Waziri mkuu wa Uturuki alitembelea Alhamisi Oktoba 29 kwa kampeni ya uchaguzi. Ahmet Davutoglu alizungumza mbele ya wafuasi wachache wa chama chake katika eneo hilo linalokaliwa na idadi kubwa ya Wakurdi.

Wafuasi hao wa chama cha Waziri mkuu katika eneo hilo la Kusini-Mashariki mwa Uturuki ni wachache, na walikua wamekusanyika mbele ya eneo walikojenga kwa mapokezi ya viongozi wa chama chao cha AKP, huku bendera za chama hicho ziklizunguka eneo hilo au kupambwa na balbu ya umeme, ishara ya chama cha AKP, chama tawala kwa miaka 13 nchini Uturuki.

Baada ya wimbo wa chama chake, Waziri Mkuu alichukua fursa hiyo kwa kuwahotubia wafuasi wake, hotuba ambayo iligubikwa na mambo ya kidini, ambapo amepinga hasa waasi wa Kikurdi wa PKK. Ahmet Davutoglu aliomba wafuasi wake kuimba kama yeye "Waturuki, Wakurdi ni ndugu! walioitenga ni wasaliti! "Kisha aliwataka wapiga kura kukipiga kura chama chake cha AKP ili kipate viti vingi kiliyopoteza katika uchaguzi wa bunge mwezi Juni uliyopita. Uchaguzi wa nchini Uturuki umepangwa kufanyika Jumapili mwishoni mwa juma hili.

Oktoba 29, ilikua siku ya siku kuu ya kitaifa nchi Uturuki, Waziri Mkuu alikua katika kampeni katika eneo la Diyarbakir. Kampeni hiyo ilikua uthibitisho: katika jimbo hilo la Kikurdi, linalojitegemea kwa kiasi kikubwa, kuna wafuasi wa chama cha AKP. "Nimekuja kwa Waziri wangu mkuu! amesema mzee mmoja mwenye masharubu meupe ambaye alikua amevaa suti ya kijadi ya Kikurdi pamoja na suruali. Nina furaha kuona yuko hapa. AKP ni chama bora na tunakipenda. "

Mfuasi mwingine wa chama cha AKP, ambaye ni Mkurdi pia, ameelezea vurugu za wiki za hivi karibuni katika jimbo hilo, akisema mabaya yote yanayotekelezwa na waasi wa Kikurdi. "Ninaishi katika kituo cha Diyarbakir, ambapo wasaliti walikuja kuharibu nyumba zetu. Hakukuwa na usalama. Watoto wangu waliamshwa na kelele za milipuko, lakini shukrani kwa polisi waliokuja kutuokoa, kwa sasa tuna amani katika eneo letu. "

Mbali kidogo watoto wa Kikurdi walichukua bendera za chama cha AKP, lakini waliihakikishia RFI huku wakitabasanu kwamba wana nia ya kuzichoma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.