Pata taarifa kuu
SLOVENIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Slovenia: zaidi ya wahamiaji 12,600 wawasili ndani ya masaa 24

Zaidi ya wahamiaji 12,600 wamewasili nchini Slovenia ndani ya masaa 24, Polisi ya Slovenia imetangaza Alhamisi hii, kiwa ni idadi ambayo ni kubwa zaidi kwa ile iliyoorodheshwa Hungary wakati wimbi la wahamiaji lilishuhudiwa kwa kasi mwezi Septemba.

Wahamiaji na wakimbizi wakivuka mpaka kati ya Slovenia na Austria, Oktoba 21, 2015 katika mji wa Ε entilj, Slovenia.
Wahamiaji na wakimbizi wakivuka mpaka kati ya Slovenia na Austria, Oktoba 21, 2015 katika mji wa Ε entilj, Slovenia. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapema Alhamisi asubuhi, jumla ya wahamiaji 34,131 walikua wameshaingia nchni Slovenia tangu Jumamosi, tarehe kulikoshihudiwa wimbi la wahamiaji na wakimbizi katika nchi hiyo ndogo barani Ulaya. Idadi hiyo ilijiongeza kwenye idadi nyingine ya wahamiaji 21455 walioingia nchini humo siku moja kabla kwa wakati huo huo, sawa na ongezeko la watu 12,676 ndani ya masaa ishirini na nne. Septemba 23, Hungary, ambayo ilifungwa mipaka yake, ilihesabu rekodi ya idadi ya wakimbizi 10,046 kwa siku moja.

Jumatano wiki hii Umoja wa Ulaya uliitisha kikao cha dharura na viongozi wa nchi za Ulaya zinazokabiliwa na wimbi la wahamiaji na wakimbizi, kwa mfano wa nchi ndogo ya Slovenia, ambayo imekua ikijaribu kuandaa, kwa shida, sehemu ya kupitia katika ardhi yake.

Marais na viongozi wa Serikali za Austria, Bulgaria, Croatia, Ujerumani, Ugiriki, Hungary, Romania, Makedonia, Serbia na Slovenia watakutana Jumapili jijini Brussels kwa kujaribu kuratibu hatua yao kwa kukabiliana na "hali ya dharura" katika nci za Balkan , Tume ya Ulaya imesema.

Umoja wa Ulaya ulitolewa wito na Ljubljana, kusaidia ikiwa ni pamoja na kuweka uzio dhidi ya wahamiaji nchini Hungary Slovenia, Serbia na Croatia, moja ya nchi kuu wanakopitia wahamiaji na wakimbizi wakielekea kaskazini mwa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.